Kuwa mwl. Tz ni tatizo, unakataliwa na jamii nzima ukianzia na Serikali kuhakikisha unafanikiwa chakula cha siku tu! Na siyo zaidi ya hapo. Sipati picha maisha yao yatakuwaje baada ya October 28, 2020!
Kuna People humu zinashadadia Mambo Utafikiri,, Hawana Akili Timamu hivi,, Hizi Harakati za Kusimamia Uchaguzi Mambo Ya sensa mbona ni Issue za walimu tangu Enzi za awamu ya Mkapa tatizo jamiiF imevamiwa na vitoto vilivyobarehe Mwaka 2020, Basi kila kitu Kwao ni Kipya.
Jana katika pitapita zangu nikapita kwenye ofisi mmoja hivi nikakutana na umati wa watu wengi nilipo ulizia Kuna nini hapa nikaambiwa Kuna usaili unafanyika maeneo haya na ni usaili wa kutafuta wasimamizi watakao simamia vituo vya kupiga kura
Kama ilivyo zoeleka kuwa wasimamizi wengi hua ni walimu wa shule za msingi na baadhi ya walimu wa shule za secondary.
Lakini nilisikitika sana baada ya kuwaona baadhi ya walimu wa chuo flani ivi tena chuo kikubwa wakiwa nao wamepanga foleni kwaajili ya usaili kwakwel nilijiuliza maswali mengi sana lakini sikuweza kupata majibu.
Je ni sahihi walimu wa vyuo kuomba nafasi za kusimamia vituo vya kupigia kura.
"If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality" - Desmond Tutu