Walimu tunapata fursa tunazichezea

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,784
Reaction score
6,183
Walimu tunapata fursa tunazichezea!

Ndio, kwa miaka mingi hapa nchini kumekuwa na matukio ya kunyanyasa au kudhalilisha walimu, na mara nyingi kesi hizo zimehusisha walimu na wakurugenzi au wakuu wa wilaya..

Wapo walimu waliowahi kuchapwa fimbo.. wapo walimu waliowahi kupigwa vibao, kutukanwa n.k

Mimi siungi mkono suala la mwalimu au mtumishi yeyote wa uma kuonyesha utovu wa nidhamu mbele ya mkubwa wake, lakini zipo njia mbadala za kushughulika na utovu wa nidhamu wa mhusika kwa mujibu wa sheria..

Kwanini nasema hii ni fursa?

Walimu wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu na morali ya kazi imeshuka kutokana na mambo ambayo kila mmoja anajua… sasa inapotokea “fursa” kama hiyo ya DC kutaka kumwadhibu mwalimu kwa kumpigisha push up au kumzaba kibao hapo ndipo mwalimu anatakiwa kuchangamkia fursa hiyo….

Niwe mkweli imefikia hatua na mimi natamani zali hilo linikute ili nitimize ndoto yangu ya kujulikana dunia nzima, naamini vyombo kama CNN, al-Jazeera, BBC, havitaacha kunitaja, na hatimaye nitachaguliwa kuwa mfanyakazi bora mpinga ubabe kazini, soon nitaanza kupata kazi ya kutoa semina kwa wafanyakazi na walimu duniani kote kuhusu namna bora ya kukataa kudhalilishwa…

Baadae nitakuwa mtoa semina wa kimataifa nap engine nikaacha na kazi yenyewe…

Nimejaribu kuwaza haya baada ya mwalimu mwenzangu kuwekwa Rumande na DC kwa ubabe tu!

Hakika natamani sana siku ya kupigwa kibao na DC,

Ndoto zangu zote hapo juu zitatimia…

Asanteni..

Tukutane uwanja wa Taifa leo jioni.
 
Wakuu wa wilaya wapumbavu kama huyo wana bahati coz nafasi niliyo nayo kwa sasa si rahisi kukutana nao lakin siku waje wajichanganye hata kwa mtu wangu wa karibu kabisa aisee huyo mkuu wa wilaya atajuta na ndio atajua kuwa kumbe kuwa na amri ya kuamrisha jeshi si lolote si chochote nawatafuta sana hao mbwa wa magufuli waje waingie anga zangu aisee !! Basi tu.
 
Kweli mkuu

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…