Wakuu mshaurini huyu mtoto

Avatar

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
11,127
Reaction score
11,938
Habarini kijana kaniomba ushauri wa kozi za kusoma kwa matokeo ya form four kwa matokeo haya biology B+, geography B, physics C, chemistry C, kiswahili C, English C, kiswahili C. Hana F wala D, lkn Advance hakufanya vizuri.

Dogo anataka kozi ambayo akisoma anaweza kujiajiri mwenyewe, nilichomwambia asome afya.

Wakuu mbele yenu hapa kuomba ideas.

Karibu.
 
Medical Lab pia sio mbaya.
 
SUA ina dip za hayo mambo natumai mkuu! au kama kuna kingine waweza nisaidia jina

Kwa case ya yak huyu mtu wako, qualifications za kusoma diploma za mifugo na kilimo zinapatikana kwenye cheti cha kidato cha sita na si vinginevyo. Advance alisoma tahasusi (combination) ipi ?
Am afraid atatakiwa kuanzia certificate.
 
Kwa case ya yak huyu mtu wako, qualifications za kusoma diploma za mifugo na kilimo zinapatikana kwenye cheti cha kidato cha sita na si vinginevyo. Advance alisoma tahasusi (combination) ipi ?
Am afraid atatakiwa kuanzia certificate.
PGM aisee, alitoka na 4 (S, S, F)
 
akafanye mitihani ya bodi ya wahasibu na wakaguzi mahesabu tanzania, ataanza na atec1,atec2 hapa anaweza anza kuijiajir kwa kuyasaidia makampuni/wafanyabiashara kufanya bookkeeping and accounting..........kuna demand kubwa ya hiki kitu, then after that anaendelea na foundation level intermediate level, na professional level,hapo atakuwa ni CPA holder, then baada ya hapo atafanya kazi chini ya mtu mwenye cpa mwenye experince ya muda mrefu.baada ya miaka miwili anakuwa full CPA yaani anapewa mhuli wa kuanza kupiga hela

atec 1and 2 mwaka 1
foundation to professional level mwaka mmoja na nusu
practicing miaka 2
total miaka minne na nusus
baada ya miaka miinne na nusu dogo atakuwa hashikiki,yaani hata wenzake walioenda kupiga bachelor watakuwa bado wanazunguka mtaani na bahasha zao

mafanikio hayaji kwa siku moja you need to plan and then follow your dream, id doesnt matter how long it takes,your dream will come true
 
aaaa
 
PGM aisee, alitoka na 4 (S, S, F)
Daah, hapo pagumu sana, wanataka bailojia kwa sababu hizo kozi ni ''life sciences'', labda tu ajaribukuomba lakini akitambua kwamba 'the odds are not on his/her favour''
 
Hii imekaa vizuri sana. Mtu mwenye bachelor, say Bsc, anaanzia level gani kaka, na huchukua nuda gani?
 
Asante sana kwa ushauri.
Inaonekana nzuri sana kinadharia...
Ada inakuaje? Kama unafahamu
 
Daah, hapo pagumu sana, wanataka bailojia kwa sababu hizo kozi ni ''life sciences'', labda tu ajaribukuomba lakini akitambua kwamba 'the odds are not on his/her favour''
Haina neno ata akianza certificate
 
Hii imekaa vizuri sana. Mtu mwenye bachelor, say Bsc, anaanzia level gani kaka, na huchukua nuda gani?
mtu mwenye bsc anaanzia either foundation level or intermediate level inategemea na course work yako ya bsc, mtu mwenye b com accounting anaanzia professional level. inachukua mwaka mmoja na nusu ukianzia foundation level, inachukua mwaka ukianzia intermediate level, inachukua nusu mwaka ukianzia professional level.

kwa maelezo zaidi nenda pale bodi ya wahasibu karibu na maktaba ya taifa ulizia upante info zaidi
 
Asante sana kwa ushauri.
Inaonekana nzuri sana kinadharia...
Ada inakuaje? Kama unafahamu
ada ndogo sina real figure but mara ya mwisho ilikuwa regstration fee ni 165,000 na tuition fee for review class ilikuwa ni 280,000
hiyo fee ilikuwa ni kwa level moja.
maelezo zaidi nenda bodi ya wahasibu karibu na maktaba kuu ya taifa
 
Shukrana sana mkuu, shukran nitafanya hivyo

SUKAH
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…