Wako wapi Makamanda aina ya James Kombe?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
6,051
Reaction score
5,952
Kifo cha mwanafunzi Akwilina ambaye hakuwa sehemu ya maandamano ya Chadema jana kinasikitisha sana. Hicho ni kifo cha pili kinachohusiana na uchaguzi mdogo wa Kinondoni.

Jana nilimsikia Kamanda Mambosasa au Murilo akionya kuwa habari za kiintelejinsia zinaonyesha kuwa kuna chama cha siasa kimepanga kufanya maandamano! Kwa nini RPC asingetumia busara ya kawaida tu ya kukaa na viongozi wa hicho na kujua sababu za hayo maandamano na kutafuta suluhisho? Au kwa kuwa Polisi wana marungu, bunduki na mabomu ndio maana hawaoni umuhimu wa mazungumzo? Popote duniani, bunduki hutumika kwa kujeruhi na kuwa, Polisi wanapotumia bunduki yenye risasi za moto maana yake wamedhamiria kuua. Kama huyo binti ikithibitika hakuwa sehemu ya maandamano, huyo RPC na Kamanda wa hicho kikosi wawajibishwe.


Madai ya Chadema ni ya msingi maana haiingii akilini uchaguzi ni Jumamosi alfajiri lkn mawakala wa Chadema hawajapata hati zao za viapo hadi Ijumaa saa 12 jioni! Mnategemea amani gani kama hakuna haki? Maandiko yanasema "haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa wote ". Kwa mauaji haya tumeaibika na kufedhegeshwa kama taifa.

Nimemtaja marehemu SACP James Kombe kwenye heading. SACP Kombe alikuwa RPC Arusha mwaka 2010 wakati Lema anashinda ubunge Jimbo la Arusha Mjini. Alfajiri ya siku ya pili matokeo yalifahamika kupitia hesabu za vituo vya kupigia kura na mamia ya vijana walifurika ofisi ya DED kusubiri DED amtangaze Lema kuwa mbunge. Hadi kufikia mchana Lema hakutangazwa na idadi ya watu iluongezeka kiasi cha kufunga barabara na kusitisha shughuli nyingine maeneo yale. Vijana walikuwa wakiimba na kupeana munkari kuwa mshindi atangazwe. Kwa busara ya hali ya juu Polisi hawakuwavamia watu wale zaidi ya kuhakikisha eneo na ofisi za serikali ziko salama huku muda ukisonga na umati ukiongezeka. Niliambiwa kuwa RPC Kombe alimpigia DED na kumwambia kuwa atangaze matokeo na ikiwa hatafanya hivyo ifikapo saa 11 jioni basi angeondoa askari wake! DED ilibidi amtangaze aliyeshinda (Lema ) na umati ule ukatawanyika kwa amani huku wakishangilia ushindi wa mteule wao.

Najiuliza, Kamanda Mambosasa na Murilo walishindwa kusoma alama za nyakati wakati intelejensia yao ikionyesha maandamano ya kudai hati za viapo lazima yafanyike ikiwa hati hazitatoka ifikapo saa 12 jioni? Waliona shida gani kufanya mediation role kama viongozi na kuwakutanisha viongozi wa Chadema na DED wa Kinondoni na kumtaka DED atii sheria? Wao Polisi si ndio walinzi wa sheria? Au kwa sababu ya kumiliki virungu, bunduki, mabomu na magari ya washawasha ndio kunawafanya wasubiri tu matukio ya fujo ili wazitumie dhidi ya uhai wa watu ambao kimsingi ilikuwa lazima wakadai hati zao kwa DED?

Damu ya binti huyo Akwilina iko mikononi mwa RPC na DED, yale maandamano hayakuwa ya lazima iwapo DED na Polisi wangetimiza wajibu wao. Nawashauri familia ya marehemu Akwilina wasiliache tukio hilo lipite hivihivi, watafute suluhisho la kisheria na kudai haki ya marehemu wao ili Polisi na watumishi wa serikali wajue dhamana na wajibu walionao kwa raia wa Tanzania.

Vv
 
. Niliambiwa kuwa RPC Kombe alimpigia DED na kumwambia kuwa atangaze matokeo na ikiwa hatafanya hivyo ifikapo saa 11 jioni basi angeondoa askari wake!
Kumbe uliambiwa!Habari za kuambiwa changanya na zako
 
Swali fikirishi. Chaguzi ndogo zinaondoka na maisha ya watu wasio na hatia, Je 2020 watakufa watu wangapi??
 
Kumbe uliambiwa!Habari za kuambiwa changanya na zako
Hapo ndio umejibu hoja! Mambosasa na Murilo damu ya huyo binti iko juu yao na irawaandama maisha yao yote yaliyosalia.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…