Wakili William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) akizungumza katika mahojiano na Jambo TV leo Machi 19, 2026 ameongelea kuhusu ucheleweshwaji wa kesi kusikilizwa licha ya serikali kuongeza ajira za majaji wapo wengi, pia kuhusu mtuhumiwa kuwekwa rumande kwa muda mrefu bila ushahidi wowote ikiwa katika kila ofisi za wakuu wa mikoa kuna maafisa wa DPP, waendesha Mashtaka wanaotakiwa kusimamia kesi.
Aidha ameongeza kuwa serikali imeongeza bajeti ya Ofisi ya DPP, Ofisi ya Mahakama na Ofisi ya Jeshi la Polisi imeongezeka huku miuondombinu ya Mahakama imeboreshwa kila Mkoa kuna Mahakama ya Mwanzo na Wilaya.
Amehoji ipi sababu ya haki za watu kuendelea kucheleweshwa?