Wakali wa kuongoza darasani sasa hivi wana hali gani kimaisha??

Wale wakali waliokuwa wanakimbiza darasani,kuanzia primary, secondary, asaivi wengi wao wameishia pabaya kwa kukosa mwendelezo wa vision zao, mwingine unamkuta asaiv ni bodaboda au shoe shine, yaani ukikutana nao roho ya huruma lazima ikuingie na kujikuta unamwachia japo chochote kimsaidie
Inferiority complex inakusumbua.
 
Maisha ni riziki anayopanga Muumba mbingu na ardhi,kwani hata kufaulu kwenyewe inategemea na mipango ya Mungu maana unaweza kusoma vizuri lakini katika mitihani ya mwisho ukapata ugonjwa ambao ukakufanya ufanye vibaya katika mitihani.Binafsi wapo watu wengi niliokuwa nawaongoza kwasasa maisha yao kila siku afadhari ya jana na wengine ni mateja kabisa.Pia kuna wengine niliokuwa nawaongoza lakini maisha yao ni Mazuri kuliko mimi,wengi wao ni wale waliotokea kwenye familia bora
Uko sahihi kabisa. Kuna mtu nimemkimbiza sana primary sasa hivi ana diploma ya clinical medicine anatoa watu mimba huko na maisha yake si mabaya. Nakumbuka alifeli form 4 wale walifukuzwa lyamungo akahamishiwa Benja Mkapa hapo.....kwa sababu kwao kuna pesa akaunga cheti then diploma. Lakini angetokea familia duni saiv naye angekuwa boda boda tu...japo naye hajafika level zangu kifedha.

So kuna wengine tumewapita na wapo tuliowapita pia.
 
Wale wakali waliokuwa wanakimbiza darasani,kuanzia primary, secondary, asaivi wengi wao wameishia pabaya kwa kukosa mwendelezo wa vision zao, mwingine unamkuta asaiv ni bodaboda au shoe shine, yaani ukikutana nao roho ya huruma lazima ikuingie na kujikuta unamwachia japo chochote kimsaidie

Kuna sababu nyingi mojawapo ni kujiamini sana na hivyo ni rahisi kushindwa vita pasipo kutarajia na hatimae historia kubadirika ghafla.
Nyingine ni kutopambana kwa kuhisi tayari ubingwa upo kumbe bado na wale wa.chini ndio daima hupambana kwa nguvu zote ili walau waponepone kumbe matokeo yake ni hayo tuyaonayo.
Isiyokubaliwa na wengi ila nayo ina mchango wake ni witchcraft kuna wengi leo wanaishi kwa akili za watu ambazowaliziiba kiuchawi wao wakafaulu wale halisi wakafeli! Baada ya kuonekana ni kipanga miaka ya awali hiyo kama huna ulinzi wa kiganga ama wa Mungu lazima wafuasi wa mwizi shetani yaani wachawi wakuibie tu ila kwa hili mtaalam mshana jnr anaweza kutuelewesha zaidi.
 
Kila mtu hapa alikuwa anaongoza!? Wa mwisho waje watupe ushuhuda wao, kama ni matajiri au hali baya!
 
Soma utafiti wa UNESCO huu kuhusu uhusiano wa umaskini na kutokwenda shule ulivyo.

UNESCO study reveals correlation between poverty and education - United Nations Association of Australia

Kifupi uwezekano wa mtu kuwa maskini unapungua kwa jinsi anavyozidi kuongeza elimu. Na kinyume chake uwezekano wa mtu kuwa maskini unaongezeka kwa jinsi kiwango cha elimu kinavyoshuka.

Usidanganye watoto elimu inasaidia kumuepusha mtu na umaskini kwa kiasi kikubwa. Matajiri wengi ni elimu zao au za wafanyakazi wao ndo zimewasaidia kufikia hapo walipo sasa.
 
Uko sahihi kabisa. Kuna mtu nimemkimbiza sana primary sasa hivi ana diploma ya clinical medicine anatoa watu mimba huko na maisha yake si mabaya. Nakumbuka alifeli form 4 wale walifukuzwa lyamungo akahamishiwa Benja Mkapa hapo.....kwa sababu kwao kuna pesa akaunga cheti then diploma. Lakini angetokea familia duni saiv naye angekuwa boda boda tu...japo naye hajafika level zangu kifedha.

So kuna wengine tumewapita na wapo tuliowapita pia.
Naona kila mtu ana aina ya vipanga wake. Yaani huyu uliyemwelezea hapa naye anastahili kuitwa kipanga? Kama huyu alikuwa kipanga basi hao wengine waliobaki walikuwa ....
 
Wale wakali waliokuwa wanakimbiza darasani,kuanzia primary, secondary, asaivi wengi wao wameishia pabaya kwa kukosa mwendelezo wa vision zao, mwingine unamkuta asaiv ni bodaboda au shoe shine, yaani ukikutana nao roho ya huruma lazima ikuingie na kujikuta unamwachia japo chochote kimsaidie
Ni kweli hata Mimi nilikuwa nashika namba moja kila mtihani kuanzia darasa la chekechea mpaka la saba lakini cha ajabu leo hii nauza majeneza Dodoma
Wakati niliokuwa nawafundisha majibu wako bungeni wengine ni wakuu wa mkoa!
Dunia haina usawa.!!!!
 
Huyo ni mmoja.. njoo Tanzania tu Anzia kwa Raisi hadi mawaziri wake au top 20 ya matajiri woote Tanzania nani alipata div 0 form 4 au form 6?
Kama wapo watakuwa wachache sana..

Na matajiri ambao hawajasoma ni kwamba walikosa chance ya kusoma sio kwamba walikua vilaza..

Utajiri na akili kichwani ni vitu vinavyoendana..ni ngumu kumkuta yule bogus wa class aliyeshinda kukariri hata definition ya matter eti amekuwa tajiri hasa labda kama aliiba hata akiwa jambazi atakufa mapema sana
You've killed it. "Hata akiwa jambazi atakufa mapema sana".. 🤔
 
Wale wakali waliokuwa wanakimbiza darasani,kuanzia primary, secondary, asaivi wengi wao wameishia pabaya kwa kukosa mwendelezo wa vision zao, mwingine unamkuta asaiv ni bodaboda au shoe shine, yaani ukikutana nao roho ya huruma lazima ikuingie na kujikuta unamwachia japo chochote kimsaidie

Yani umeongea fact kamanda...naweza nikasema asilimia kubwa au wote kabisa maisha yao duni ukilinganisha na wa primary...na hao hao wenye mavyeti wameajiriwa na wa darasa la 7...

Biashara ni akili na ujanja tu...uliweza kuwa unabukua class lakini ktk biashara ni ZERO kabisa...
 
Back
Top Bottom