Zamani ilikuwa mtu ukipata wageni mnakaa mnapiga stori, mnapeana habari za miaka tele na kufurahi pamoja. Siku hizi hali ni tofauti. Mkishasalimiana tu kinachofuata ni kukodoa macho kwene tv. We unajaribu kuanzisha topic ili angalau muongee lakini wapi bwana.. wageni macho pima kwn screen. Wengine ndio kwaanza wanashika rimoti na kuanza kuchagua channel wanazopenda wao. Jamani, mmekuja kunisalimia au kuangalia tv? Mi kuanzia sasa nikipata wageni nazima tv!
ukizima tu nasepa
hahahaaaa eti nimekuja na mkanda wa mitun chakarabotha ha ha mada zingine ni vunja mbavu tu. Hebu niwashie TV huko, nimekuja na mkanda wangu wa Sarafina.