SERIKALI YA JPM YABORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama ameliambia bunge kuwa serikali ya awamu ya 5 imeboresha kwa kiasi kikubwa maslahi ya wafanyakazi nchini.
Amesema maslahi ya wafanyakazi yaliboreshwa ni pamoja na barabara nzuri, huduma bora za afya, maji na umeme.
Amesema si kweli kwamba maslahi ya wafanyakazi ni nyongeza ya mishahara tu, bali hata barabara nzuri wanazotumia, maji safi ya bomba, umeme hadi vijijini na huduma bora za afya wanazopata.
Kuhusu nyongeza ya mishahara amesema wafanyakazi waendelee kuwa watulivu kwa kuwa serikali itaongeza mishahara ikishakamilisha mipango yake ya kiuchumi.!
Sent using
Jamii Forums mobile app