bakundande jr
JF-Expert Member
- Oct 22, 2021
- 507
- 674
Moja kwa moja kwenye mada.
Kutokana na sababu tofauti kumekuwa na panda shuka ya bei ya bidhaa tofauti kuanzia vinywaji hata vyakula.
Kitu cha kushangaza ni kuwa wafanyabiashara wanakuwa wepesi kubadilisha bei ya bidhaa pale wanaposikia bidhaa hiyo imepanda bei hata kama ndio ametoka kununua bidhaa hiyo kwa bei chee jana yake ila imekuwa tofauti pale ambapo bidhaa hushuka bei.
Kwa mfano upande wa vinywaji hususani soda imepita kama wiki naona matangazo na mabango ya kampuni flani kushusha bei ya vinywaji vyake ila kila nikienda kununua bidhaa hizo nakuta bei ni ile ile. Kitu cha kushangaza zaidi ni kuwa kwenye duka hilo hilo unaweza kuta bango ambalo lina onesha kushuka kwa bei ya bidhaa husika.
Sasa kama bado mnakuwa na mzigo mkubwa kwanini msikatae kuweka hayo matangazo?
Kama leongo ni faida wasiwe wanaweka hayo mabango ya punguzo la beiHapo lengo kuu ni kupata faida tu ukizingatia hii panda shuka ya bei za bidhaa sion kama wafanya biashar wanamakosa
Kutokupunguza sio tatizo, tatizo ni kuweka bango linaoonesha bei ya bidhaa halaf unauza bei tofauti.
Kutokupunguza sio tatizo, tatizo ni kuweka bango linaoonesha bei ya bidhaa halaf unauza bei tofauti.
Hawezi ona shida kununua soda buku kwenye hotels kubwa coz ndio bei inayotambulika sehem hiyo
Almost yote yanafanyika mambo ya namna hii
Mkuu hapo kwenye suala la faida sipongi ila ni kwanini uweke tangazo lenye bei tofauti na bei unayouza???Lengo la mtu kuweka pesa yake kwenye fremu ni kupata hela ndugu
Tatizo la wateja wengine wanataka wafanye mahesabu ya faida yako wakupangie eti faida ya mia moja inatosha nyingine yote ya nini..
Hajui kwamba kufuata mzigo ni gharama pia Kodi inahitajika tofauti na kwamba pia unakuza biashara yako