Kwanini Serikali isikae na wafanyabiashara wakazungumza na kufikia muafaka au mpaka waje wamarekani na umoja wa Ulaya waje waishauri Serikali kama wanavyofanya Sudani na Somalia?
Ni kweli kabisa...waache wagome hata mwezi mzima wakitaka...lakini hiyo mbinu ya kugoma ili kuishinikiza serikali imepitwa na wakati.
Na kodi watalipa tu hakuna kukwepa..na lazima ifike mahali serikali ikatae kuburuzwa na hivi vigenge vya wajanja wajanja wanaolilia huruma ya serikali ili wapate faida maradufu..wakati mlaji wa mwisho hajawahi faidika na iyo nafuu wanayopewa...waache tabia za kupe na papasi...
Taarifa za chinichini ni kuwa kesho hata vyombo vya usafiri havitafanya kazi, mkoani mbeya kuna vipeperushi vimesambazwa juu ya hili la mgomo, tangia ijumaa maduka hayajafunguliwa
inashangaza sana mtu kuhamasisha wenzake kukataa kulipa kodi wakati huo huo akiikosoa serikali yake kwa kutompatia huduma bora . watanzania hatuna hulka ya kupenda kulipa kodi.