Wadada

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Kuna tofauti kubwa kati ya mwanaume kukutambulisha kwao na kujitambulisha kwenu.

Wanawake wengi wanapotaka kuishi na wanaume ambao hawajafunga ndoa nao au wamezaa nao wana kitu wanakuambia “Njoo basi ukajitambulishe kwetu?” Mwanaume akishajitambulisha basi hujisikia rahaa na kusema “Kwetu anatambulika!” Wengi hujiona kama mke kabisa, lakini ushawahi kujiuliza je mko wangapi ambao ashaenda kujitambulisha.

Nirahisi sana kwa mwanaume kujitambulisha upande wa mwanamke, tena wakati mwingine hata kutuma ndugu kwenda kuongea, nirahisi kwakua anaweza kujitambulisha sehemu hata kumi, akajitambulisha kwa wanawake kama kumi hivi na wala asijali.

Lakini kama mwanaume anatokea katika familia inayojielewa basi ni ngumu kuwatambulisha wanawake zaidi ya mmoja kwa Mama yake.

Mara nyingi atawatambulisha kwa Dada zake na Kaka yake mmoja wale watu ambao ni washikaji lakini si kwa wazazi wake.

Ingawa haimaanishi kwakua kakupeleka kwao ndiyo kashakuoa lakini una afadhali kidogo kama kakutambulisha kwao kuliko kujitambulisha kwenu.
Acha kujimilikisha mwanaume na kujiona mke wake kwakua kajitambulisha kwenu, ukiona mwanaume ni rahisi rahisi kujitambulisha basi jua hiyo ndiyo tabia yake na inawezekana hajajitambulisha kwenu tu.

Mwisho wa siku ondoka kwenu kwa ndoa haya mambo kwetu anajulikana, kashanipeleka mpaka kwao yashapitwa na wakati wengi siku hizi hawajali!

Nimeileta kama nilivoiokota!
 
Umenena vema mkuu, hili ni jambo la kuzingatia mno, maana wadada tumekua watu wa kujisahau sana.

Kuwaamini wanaume bila kuwachunguza ni kosa linalotufunga wengi, yaan wamekua ni matapeli na waongo wa kutukuka.

Mungu atupe macho ya kuona na akili ya kutambua jema na baya na ili tuweze kuushinda huu mtihani pia maana kwa akili zetu hatutaweza.
 
Ujumbe umewafikia walengwa
 
Mpaka mkifikia kutambulishana ni hatua nzuri...mm siwezi kujitambulisha kwa ajili ya kuosha rungu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…