Wadada mjiheshimu.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Wadada mjiheshimu mavazi mnayovaa siku hizi yanawadhalilisha, unafikri ukivaa vizuri hamtatongozwa mnakera sana.
 
Ubaya zaidi ni kwamba wanao furahishwa na hayo mavazi ni wengi kuliko wanao kerwa na ndio maana wanaendelea kuvaa!
Ukiona service bado hiko sokoni basi ujue wateja nao wapo!
 
Ukitaka kumuheshimu mtu utamuheshimu kwa kivazi chochote kile. Hata skimpy bikini. Tunaona watu wako na vibikini in the Azores, Copa Cabana, Costa Del Sol,South of France etc, na wanaheshimiwa kwa nafasi zao.

Wazo kwamba mwanamke asiheshimiwe kwa sababu kavaa vibaya ni barbaric, hatujui historia yake na sababu zilizomfikisha hapo, pengine ni mgonjwa -nishasema maradhi ya akili ni mengi, lakini mpaka mtu aokote makopo ndo ajulikane- pengine yupo kazini na kazi yake inamtaka avae hivyo, pengine ni mwanaharakati wa kuleta mawazo mapya katika jamii yetu.

Na hapo katika mawazo mapya katika jamii yetu naona kuna unafiki mwingi sana wa Waafrika kujifanya prudes, wakati mavazi yetu ya asili ni vibwaya, kinadada wanatembea chuchu nje mpaka 1950's just outside of Dar! I am not talking about some exotic Mswati dance.

Sasa hayo mavazi yaliyofikia tamaduni zetu hizi ni yapi zaidi?

Heshima haiji kwa mavazi. Narudia, ukitaka kumuheshimu mtu utamuheshimu kwa kivazi chochote kile

Na usipotaka kumuheshimu, hutamuheshimu hata akijipiga ushungi wa Niqab au guo za kitawa.

Unaweza kutaka kuweka zulia dunia nzima ili usikanyage ardhi.

Au unaweza kuvaa kiatu na kufikia lengo lile lile kirahisi.

Usitake kuweka zulia dunia nzima kwa kazi ambayo kiatu mguuni mwako tu inaweza kukifanya.

Kama unapenda heshima waheshimu wote, wanaovaa vizuri na vingine.
 
So vague. Mavazi gani hayo yanayokunyima raha mpaka kuja kuanzisha thread?
 
Wadada mjiheshimu mavazi mnayovaa siku hizi yanawadhalilisha, unafikri ukivaa vizuri hamtatongozwa mnakera sana.
Wakaka mjiheshimu, hizo suruali zenu mnazovaa vikiwa zimeacha ma.ta.ko nje zinawadhalilisha. Hatuna haja ya kuona mifereji ya ma.ta.ko yenu wala pichu zenu. Mnakera sana nyie
 
Asante sana,
Hawa jamaa huwa wananikeraga sana, huwa natamani ningekuwa na uzalendo kama DC Mnali niwaweke Viboko kabisa!


Wakaka mjiheshimu, hizo suruali zenu mnazovaa vikiwa zimeacha ma.ta.ko nje zinawadhalilisha. Hatuna haja ya kuona mifereji ya ma.ta.ko yenu wala pichu zenu. Mnakera sana nyie
 
Wakaka mjiheshimu, hizo suruali zenu mnazovaa vikiwa zimeacha ma.ta.ko nje zinawadhalilisha. Hatuna haja ya kuona mifereji ya ma.ta.ko yenu wala pichu zenu. Mnakera sana nyie

Naona hii inageuka kuwa vita ya jinsia.

Au kama wengine wanavyoweza kusema, sanaa duni.

Kuna tofauti kati ya kuzidisha na kujumlisha hasi.

Wewe unazidisha sehemu ya kujumlisha!

Love over hate, understanding and serenity over prejudice and callous excitement.
 
Fantastic,marvelous,absolutely right,outstanding yaaani sijatosheka na maneno yote hayo hapo juu niliyosema kuhusu huu mchango wa kiranga i like that
 
Waacheni bhana wanatuonyesha utamu utamu utamu.............!
ile Kitu tamu bhana ukiona paja unaendelea kufikiria zaidi kilichoko juu ya paja aaaiiisseeeee....................:rockon:
 
Huko Lesotho wanawake hawavai nguo kabisaaaa!!! chuchu inafichwa kwa kunatisha kijipande kidogo cha Big G iliyotafunwa.
 
Mtoa mada hebu tuambie mavazi halisi na asilia ya mwanamke wa kitanzania/kiafrika ni yapi tuvae?
Maana watu wanasahau sisi nguo zetu zilikua vibwaya kutokana na hali ya hewa ya africa.wazungu kutuletea haya mavazi imeshakua ndio mila yetu kebooo
mila zetu ni vibwaya ,kama mnataka tuzae hivyo sawa
 
Naamini siku watanzania tukiacha upuuzi wa kujadili maisha ya watu tutaendelea. Vazi kanunua kwa ela yake na kavaa yeye, wewe linakuhusu nini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…