Wachezaji kubadilishana jezi.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,709
Reaction score
1,735
Nimekuwa natafakari jambo hili kitambo sasa kuwa kwa nini wachezaji mpira (hasa soka) mara mechi iishapo hubadilishana jezi na sijaona mchezaji akibadilishana na refa wake wakati wote wameshiriki mechi moja? Huu ni ubaguzi.
 
Kwanza, jezi ya refa inakuwa na ile kadi nyekundu kwa hiyo refa anaogopa akibadilishana na mchezaji huyo mchezaji anaweza kumpa red hapo hapo.

Pili, tatizo lingine ni huyu jamaa hapa kwenye picha. Anawachimba biti marefa. lol



Lakini pamoja na biti la Fergie, wapo baadahi huwa wanabadilsihana jezi kimtindo.

 
Mkuu, jezi hubadilishwa mechi ikiisha mbona! Hivo kadi zake anaweza kuzitoa na kukaanazo mkononi ati.
 
Refa akibadilishana jezi atabadilishana na nani???

Maana kwa mfumo wa soka refa hatakiwi kuonesha inclination na upande wowote ule...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…