Absolutely. Umepatia vizuri sana mkuu.
mbona unawasahua walimu... siku hizi wanaitwa shemeji madarasani!
Tangu nizaliwe sijashudia Tanzania ikiwa na njaa ya kiongozi kama ilivyo leo hii. Hadi inatia aibu. Raisi ameshindwa katika secta zote. Sheria hakuna, elimu sifuri, matibabu yai, miundombinu usiseme. Tunaenda wapi watanzania? Yaani hadi inatia huruma nchi haina waziri hata mmoja vilaza kibao utendaji sifuri kabisa. Yaani jamani tunapitwa na Waganda ambao walikuwa na vita za wenyewe kwa wenyewe miaka yote. Wameamka wanasomesha watoto wao sisi tunachekeana na vilaza wa kutupwa. Ni lini tutawawajibisha hawa wezi wasiojali taifa hata chembe kazi kukwapua tu raslimali zetu huku wakituacha tunaangamia?
Kuna hili la ualimu kuwa kazi ya watu waliopata alama za chini nadhan nalo kuna haja ya kuliangalia upya ingawa ni gumu sana wengi wetu kulizungumzia. Haiwezekani utegemee mwalimu wa Hisabati afaurishe watoto wapate A wakati yeye mwenyewe mwalimu enzi zake alipata Hisabati D au alifail kabisa.
Mfumo wetu unafanya elimu ni sehemu ambayo waajiriwa wake ni wale waliopata alama za chini wakiwa wanafunzi. Hivi hapo unategemea nini hasa????Mbona vyuo vikuu wameweka GPA za juu kama kigezo?? Kwann wasiweke GPA za chini pia kama kigezo cha kuajiri wahadhiri??? Au elimu ya chuo kikuu haina uhusiano na hii elimu ya huku chini????Au tunategemea miujiza ipi mwalimu wa sekondari aifanye katika kufundisha kitu asichokiweza?????
Serikali inadhan nini kinazuia mtu aliyefauru vizuri kukimbilia ajira za ualimu???Mtu aliyefauru anaona kuwa mwalimu wa sekondari sio option ya ajira maana anaona kwenda huko ni kujitaftia umaskini. Kama mishahara ya walimu wetu ingekuwa minono kama ile ya TRA au kama wa Livingstone Lusinde kibajaji hiv unadhan wale wenye Div I point 7 msingewaona huko?????Au kama mishahara ya walimu ingekuwa kama ya Politicians unadhan wakina Mwakyembe wangekuwa na haja ya kukimbia chaki???? Nani anapenda umaskini???
Hatuhitaji microspic eyes au rocket scientists wala tume kama Pinda anavyotaka kutuaminisha katika kubaini matatizo ya walimu nchini. Vilio vya kuporomoka kwa elimu havijaanza leo, mengi yalishasema serikali ikaweka pamba maskioni. Waziri mkuu ajiulize huko huko nyumbani kwake, maslahi anayoyapata je yanalingana na ya mwalimu???? Au anataka kusema yeye analipwa hivyo kwa vila amesoma sana?? Kwa vile anaitumikia sana Serikali yetu au kwa vile mzalendo sana???? Inahitajika Political will tu kuiinua sekta ya elimu.
Kwa nini serikali inahisi walimu hawapaswi kupata maslahi bora??? kama nyumba nzuri, afya bora, allowances nzuri na mishahara minono??? Kazi ya ualimu ni ngumu sana kuliko hata kukusanya kodi au kuratibu michango ya NSSF, PPF,PSPF, ni ngumu kuliko jeshi maana ina implication kubwa sana kwenye mustakabali wa taifa husika. Ni kazi inayohitaji moyo wa kizalendo kuifanya na upendo wa dhati wa kiuzazi kwa mwanafunzi unayemfundisha.
Itoshe kusema, kimsingi anguko la elimu hapa nchini limechangiwa kwa kiasi kikubwa na serikali yetu. Sasa nini kifanyike nadhani wadau humu mtaweza kuweka mitazamo vizuri! Mana kulaumu tu bila kutoa suluhu pia si busara.
Pamoja na walimu kutopata haki zao lakini tatizo lililopo ni kutokana mfumo wa elimu ulivyo tangu chekechea hadi Chuo Kikuu.Moja chekechea lazima wawe na muundo wao wa kuanza kujifunza.Zamani elimu ya awali ilikuwa katika mfumo wa 3Ks maana yakeKUHESABU,KUSOMA na KUANDIKA ndio sababu huko kwetu shamba tulianzia kuandika kwenye udongo-kibao na baadae daftari.:yo:Tulianzia kuhesabu vidole-kuhesabiana mstarini vijiti na baadae tebo ambayo kila daftari ilikuwa nayo.Kinyume na sasa mtoto wa elimu ya awali anabeba vitabu zaidi ya kilo tatu,anajifunza nini?Kwaa mtindo huu mtoto anakariri tu bila kujua anachokalili kilipatikanaje kwa elimu yake aliyonayo.Kwa kutofuata mbinu za ufundishaji ndo maana watoto wengi wanadumaa kiakili hadi elimu ya juu.Kama janga lilotupata 2012 haiwezekani mwanafunzi akashindwa kujibu hata swali moja .Mitaala mibovu ndo maana hata shule za binafsi na zenye vipaji wote kushnee.Wananchi tunamlaumu Ms Ndalichako kwa watoto kufeli mlitaka afanye standardization ili washinde bila kufaulu .Tumshukuru huyo mama kwa sababu ameonyesha zaili jinsi gani elimu yetu iko duni inatakiwa ifanyiwe ukarabati mnono.mazara ya kuiba mitihani na kununua ufaulu unajionesha kwa sasa ni jinsi gani tunavyokosa ajira kwa visingizio kibao.Hata tukiodoa Kawambwa hakuna jipya kwa sababu mitaala yote kaikuta.Wakati umefika tusiwe na akili mgando tuwe na mageuzi kwenye sekta ya elimu na matunda tutayaona.Watanzania tunao wataalamu kibao mpaka wengine wanapew uraia ,uwaziri nk jaribuni kuwarudisha ili wakarabati nchi yao kwa sababu msingi wa elimu zao ni tanzania.Hapo awali enzi za Nyerere Tz ilikuwa inaongoza kwa elimu Africa ,jaribu kuperuzi nyaraka zinazo husu Chuo kikuu cha dsm ,Ihungo,Nganza,Tanga School,mzumbe,Kahororo,Nyakato,Nsumba,Galanos,Bwiru,Kib :wink:
Mkuu umemaliza, kama inawezekana hiyo tume ya Pinda ipitie hiki kipande.
inamaana na hao walimu wa sekondari waliotoka vyuo vikuu ni failure au walipata division 4? au hawa wa division 4 mnaowaita failure ndo wameanza kufundisha kuanzia matokeo yalipoanza kushuka 2010? na hapo nyuma waliokuwa wanafundisha primary walikuwa na division ngapi? na kwani hawapo mpaka sasa?nadhani mkijibu haya maswali mtapata mchanganuo mzuri.
Nina uhakika unaelewa vizuri utaratibu wa elimu ya Tz, mwalimu yeyote awe wa Certificate, Diploma au Degree, ni chaguo la Division za chini. Hii ina maana mwanafunzi ambaye hakua mzuri darasani ambaye sasa ni mwalimu anafundisha wanafunzi kwa kiwango hicho cha uelewa mdogo. Sasa basi, angalia hiyo hali ikijikusanya kwa miaka tuseme 10, kiwango cha uelewa kitazidi kushuka sana.
Ni jambo linaloeleweka kwamba katika darasa, wanafunzi wanaopata Div 1 na Div 2 ni nadra sana kusoma ualimu (sidhani kama wapo wanaosoma ualimu). Sasa hawa ndo tunaofahamu kwamba uelewa wao uko juu zaidi na hata ktk discussions za mashuleni unakuta hawa ndo wanawaelekeza hao wanaopata Div 3 na Div 4 (hao wa Div 0 tusiwaongelee kabisa) na wakitoka hapo wanakwenda kusoma ualimu waje wafundishe unategemea nini???.
Kwa wale wa Degree hata kama hawakupata Div 4, lakini bado ufaulu wao si mzuri kama wale wanaochukua fani zingine kama Wahandisi, Madaktari, Wahasibu, Wanasheria nk. Hatutegemei mtu amepata Div 1 point 3 hadi 9 Form Six aende University akasome Education (kama amewahi kutokea naomba unifahamishe).
Sasa basi ukilimbikiza kwa muda mrefu kama nilivyosema hapo juu au hata miaka 20, kwa wale wanaoelewa kidogo kufundisha, unakuta idadi ya wanaoelewa kidogo inazidi kuongezeka. Kwa nini Lecturers wanabakizwa wale waliofanya vizuri??? kwa sababu wanafunzi wanaokwenda Universities ni wale wenye uelewa wa juu hivyo ukimbakiza mtu aliyepata PASS sidhani kama atawezana na mwanafunzi aliyepata Point 3.
Ninaamini nimeweza kukupa majibu ya maswali yako, ingawa haikua nia yangu kuzungumzia ufaulu wa walimu katika ngazi tofauti (kwenda kusoma Certificate, Diploma na Degree) lakini imenibidi kufanya hivyo ili kukidhi haja ya maswali yako. Hata kama nawe unasoma ualimu au ni mwalimu tayari, nia yangu ilikua ni kueleza hali ya elimu ya Tanzania, hivyo nitaomba nisieleweke vibaya japo naamini hata wewe unafahamu hayo niliyoyaeleza.