Wachanganyikiwa........!

Shagiguku

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
409
Reaction score
138
Baadhi ya watanzania wamechanganyikiwa na uchaguzi wa kenya.

Katika hali hiyo wapo watanzania ambao wanasema watanzania HATUNA cha kujifunza kutokana na uchaguzi huo.

Na watu wengine wanasema watanzania TUNA KITU cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa kenya.

Na mimi nasema watanzania TUNA KITU cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa kenya, haiwezekani uchaguzi kama huo tukose kitu/ jambo la kujifunza.

Baadhi ya mambo ambayo tunajifunza kutokana na uchaguzi wa kenya ni haya hapa yafuatayo, na mengine wewe kama great thinker utayaongeza hapo chini...!

1. Kwamba matumizi ya njia za ki-elektroniki siyo mara zote yanaweza kurahisisha kazi katika uchaguzi.

2. Kwamba inapotokea njia za ki-elektroniki zimekwama basi tuwe wavumilivu kwa kusubiria matokeo kupitia njia za jadi za mababu zetu (kuhesabu kwa vidole)

3. Kwamba njia za ki-elektroniki zinaweza kutumiwa na baadhi ya wajanja wenye pesa (wagombea urais) kuwatumia vijana wetu wa IT (teknolojia ya habari na mawasiliano) ku-haki (kuiba) njia zinamopita hesabu za kura kabla ya kufika kwenye kituo cha tume ya uchaguzi na kuzichakachua (kuzi-DOCTOR) humo njiani na baadaye kuzituma zikiwa zimepinduliwa au kumfanya mgombea mmoja kura zake zisiwe zinasogea kwa idadi kwa kuongezeka kwa muda wa masaa kadhaa.

4. Kwamba inawezekana pia kuhama kutoka DIJITALI na kwenda ANALOJIA na tena usitupe mbachao kwa mswala upitao. kuna watu wanaamin kwamba kila kitu kinachofanywa kwa kompyuta ndicho haswa cha ukweli na kile kifanywacho manywale (kwa mikono) eti kinakuwa kimepitwa na wakati.
kumbuka marekani waliwahi kurudia kuzihesabu kwa mkono baada ya dijitali kufeli.

5.................................................................................................................!

6................................................................................................................!

7................................................................................................................!

8.............................................................................................................!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…