Hawakupewa nafasi ya kuijadili kwa pamoja ili wapeane hoja za kujitetea ndo maana wakapewa muda wa kuikariri na kuitoa kiuzalendo.
Wanaposema kuwa uwe muungano wa serekali 2 ulioboreshwa; hayo maboresho mbona hakuna hata kamati moja tu kati ya hizo 12 iliyotoa mfano wa maboresho hayo? Zaidi sana ni kuiambia Zanziba kuwa Gas na Petroli hatutaiweka chini ya muungano?? Ili Zanziba wazidi kupewa hallua?? Ama kweli, Tz kuna mambo mapya kiila siku. Hamuoni huku ni kuitukana Zanziba kuwa wao wanalilia sukari tu??
Umeme wameutumia miaka yoote, Mtanganyika ndo anamlipia, Mafuta tunayapitishia bara, yanaenda kwao ka yametoka Pemba tu, Serekali ya Muungano jamani ni ipi hiyo iliyojiunga na Zanziba??
Kila mjumbe akisimama anadiriki kusema kuwa kuwe na Serekali inayoitwa ya Muungano na Serekali ya Zanziba. Hainiingii akilini kuwa hiyo nchi inayoitwa Serekali ya Muungano ni ipi na ya Zanziba ni ipi. Hii ya muungano imetoka wapi bila hiyo Zanziba???
Nimeshaleweshwa na sauti hizi za wenyeviti wa kipekee wasiojua hata wanachokisema. Nasema, Semeni mtakavyo ila kuna siku, Tutaenda UN kuudai uraia wetu mlio tunyang'anya kwa utapeli. CCM Oyeeeee.