Nawashangaa sana hasa hao vijana,nilichogundua kumbe mfumo hapa ndiyo tatizo,si wazee wala wa ukongwe ndani ya chama bali ni ule ugonjwa unaoitwa(MKNC) Maslahi Na Chama Kwanza.
Baada ya kulaani na kushindwa kusaini hoja ya zito kabwe ya kutokua na imani na waziri mkuu wakimuogopa mkuu wa nchi kumbe naye rais alikua anafurahia wabunge walivyokuwa wanajadili.wadai wangesaini wangejiongezea umaarufu wa kisiasa kwenye majimbo yao kwa kuonekana wapiganaji.source greatethinker
Pamoja na ujinga wa hao wabunge kushindwa kusoma alama za kisiasa, lakini na viongozi wa chama chao wanawapiga chenga za kisiasa pia. hakukuwa na dalili kuwa chama kama chama kina msimamo gani katika hili. Mimi nilikuwa Dodoma na kilichokuwa kikionekana ni kutokuwepo kwa msimamo kwa viongozi wa juu wa CCM na serikali. Walikuwa wanayumbishwa kama bendera. Mwanzoni Zitto alipoanzisha hoja ya vote of no confidence, waliona kama masihara, walioona hoja inaanza kuwa na mashiko, ndio wakaanza kuhangaika na wakaja na suluhisho la zima moto.Ni kweli wabunge wengi wa ccm walidhan ni wimbi tu litapita ndio maana wachache walioona mbali walitia sahihi zao.
Na sasa wachache hao wanajivunia uhuru wao kamili ndan ya ccm.
Hata hivyo waliogopa ni uvivu wao tu wa kufikiri kwan hawajachaguliwa na ccm bali ni wananch wanaopaswa kuwaogopa ama kuwatii na sio viongozi wa ccm.