Wabunge kabla ya ufisadi

mukizahp2

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
705
Reaction score
378
[h=3]WABUNGE KABLA YA UFISADI[/h]
Kabla ya ujio wa ufisadi uliotutoa kwenye ujamaa na kujitegemea hadi kwenye unyama na kujimegea hali ilikuwa hivi yani wabunge walikuwa wanapanda gari moja (Basi) kuelekea Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Je leo hali ikoje kwa wabunge wetu na unadhani kwa wao kuwa kama miungu watu wataweza kuwatumikia wananchi kiukweli?
​
Ndugu yangu hali ni mbaya na inatisha sana na sababu ni viongozi kuwa mbali na wananchi waliowapigia kura,leo hii hakuna wa kupinga ongezeko la nauli kwa mtanzania kwa sababu wamiliki wa vyombo vya usafiri ndio watoa maamuzi.

Mwananchi wa leo ana kazi ya ziada katika kuhakikisha viongozi wake wanamjali na kumthamini kwa kumtetea katika uonevu wowote na kumsaidia kuondokana na hali ngumu ya maisha na hapo ndipo ninaiona haja ya kila mmoja wetu kujihoji na kuchukua maamuzi sasa.​

Posted by NEW ERA LEARNING CENTER at 4/10/2013 01:46:00 PM
 
Hivi mabasi dezine hii bado yapo? je walisafiri kwa lazima au hiyari? je wakati ule kigezo cha kuwa mbunge kilikuwa nini? hali ya nchi ilkuwaje kisiasa na kiuchumi? je ni kweli walifanya kazi kwa moyo na nia njema au ndio walianzisha haya tunayoyaona kwa sasa? wakati mwingine huwa nashindwa kuiona tofauti ya zamani na sasa! hivi zamani ni lini? na sasa ni lini in big picture???/ je toauti ya zamani na sasa ni katika picha tu au kuna kingine/vingine? au ni namba tu ya miaka? je zamani ni kama Analogia na sasa kama digitali, mbona vyote vinafanya kazi sasa? vina uhusiano gani? kabla hajafa Nyerere alipondwa sana na hao aliowanyima nafasi na wengi wenye kutaka vya fasta fasta! sijui ndo wa zamani hao, miongoni mwao wapo hadi hii inyoitwa sasa na wanamsifia. sijui nimuamini au kumsikiliza nani? Muarobaini bado mchungu huu!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…