Wabongo wanahadhirika SA.

mkenya mkweli

Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
37
Reaction score
2
juzi juzi nimekwenda south africa mji wa durban kutembaa,basi ikawa nitakwenda kutembea bandarini ili nionyeshwe bandari kubwa africa.

nimewakuta wabongo wengi ajabu halafu wachafu sana wanalala kwenye park karibu bandarini.niliskia wanongeo kiswahili basi nikawakaribia, katika mazungumzo niliwauliza wanafanyaje pale,eti wanangoja kupanda meli waeende zao ulaya.wengine eti wamengoja miaka kumi pale bandarini.wote wale walikuwa watanzania.sijui kama serikali yenu Tanzania inajua kuhusu hawa jamaa zetu,maana ni wengi ajabu.
 
Mhhh, sasa huko ulaya wakafanye nini.Hukuwadadisi zaidi?
 
ulaya gani wanataka kwenda?? hii ulaya ya nchi za scandinavia ambazo hata mimi nilikuwa huko? au kuna ulaya nyingine bara lingine? lol masikini wee .. wangejua yanayoendelea ulaya wangerudi zao bongo na kuanzisha miradi ya kuanza kula maisha.
hivi haa jamaa wanajua mkuwa europe(wazungu) watu wanajiua kwa kukosa pesa ya kula?
 
hakuna wakenya huko?
 
acha wajilipue..nyie komaeni na mafisadi kwanza....watarudi tu end of the day!!
 
Warudi nyumbani kufanya nini!! Wache wakae huko huko watafute maisha...wakirudi Bongo hakuna deal sana sana wataongeza idadi ya vibaka!!
 
Hilo ni somo tosha kwa vijana wa kibongo wanaotaka kwenda south eti kutafta maisha,wenzenu wanaishi maisha ya kinyama hayo zaid ya miaka 15,nibora kubaki bongo uuze juice upate mlo wasiku kuliko kwenda kuhangaika ugenini.
 
Kinshasha Wabongo wapo kibao, Capetown wapo kibao, Nairobi wapo kibao, Harare wapo, Accra wapo kibao - Wabongo wako all over Africa wanatafuta maisha! Waache waendelee kuhangaika kwa ajili yao na familia zao - Labda kama umezoea udaku!

After all, wewe ulienda Durban "kuonyeshwa bandari... blah blah.."?
 
hakuna wakenya huko?

Kusema kweli,sikuona mkenya,nimefanya kuwauliza wapi kunapatikana wakenya wakadai wakenya wapo lakini kidogo ngumu kuwapata.wakanionyesha baa ya mkenya moja na kuniambia usiku usiku hivi wakenya wanapatikana pale.

hao wabongo wanadai eti ni mabaharia
 

ndio kinshasa wapo,harare wapo lakini wanaishi vizuri.sio wachafu wakunuka na vibaka.na sio udaku,ila am trying to put the matter on the table,may be there are some politician in this forum, good Samaritans or even authority whom they can consider this issue and put it forward to the necessary body/establishment per se
 
Nenda Summit Club pale Johannesburg ukaone mabinti Wa kikenya walivyojipanga kuuza miili yao usiku. Usikalie tu kuwasema wabongo dada zenu wanawadhalilisha sana
 
Nenda Summit Club pale Johannesburg ukaone mabinti Wa kikenya walivyojipanga kuuza miili yao usiku. Usikalie tu kuwasema wabongo dada zenu wanawadhalilisha sana

Jamani si kusema kwa ubaya.nisharudi zangu kenya.

kitu chengine umalaya upo kila mahali,hata hapa kenya malaya wengi ni wabongo na waganda. lakini issue hapa ni hao mabaharia kama vile mwingine amesema.hili ni soma tosha tusije takakimbila ugenini kumbe maisha huko ni mabovu.
 
Kama ni kuadhirika kimaisha sio SA tu hata ulaya wapo watanzania wanaadhirika kweli kweli. Juzi juzi nilikuwa London,jamaa moja aliingia kwenye Mgahawa, akaangaza angaza macho, alipotuona na kutusikia tukiongea kiswahili wakati tunakula (tulikuwa waTZ 2 na Mkenya moja) akaja kutuomba chakula. Ukweli sikuamini macho na masikio yangu, lakini huo ndio ukweli uliotokea.Baada ya kumdadisi anatoka wapi hapa TZ akatueleza kwamba anatoka DSM sehemu za Ubungo Msewe
 

The authorities have failed to address the povercy and unemployement isssue(s) at home, in-country, how the hell do you think they can fix these issues across the border? - thousands miles away!?

When did you last visit Kibera? Are these Wabongo worse off?
 
hahhahaha!! nilitegemea jibu kama hili
mboona hata mimi last time nilienda jo'burg nikakutana na mmbongo anamiliki petrol station.
 
Nenda Summit Club pale Johannesburg ukaone mabinti Wa kikenya walivyojipanga kuuza miili yao usiku. Usikalie tu kuwasema wabongo dada zenu wanawadhalilisha sana

kakurpuka kuleta taarifa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…