Kuweni na akili zilizopevuke(matured) nyie mnaooitwa wasomi wa Tanzania. Hivi can you tell us, what kind of contribution hii thread inatoa kwa ukuaji wa elimu ya Tanzania. Thread za namna hii zimekuwa ni nyingi sana, ni kibaya zaidi hata watoa thread wanaonekana uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.
Hata hii thread yako ina mtitiririko utadhani ni mtoto wa darasa la kwanza..jaribu kukua hasa kwenye fikra zenu, haya mnayoandika hapa, yanasomwa na watanzania wengi na hata ndugu zetu wa karibu yaani EA. Kwa mawazo kama haya nadhani ndio maana wasomi wa Tanzania tunaonekana wa kawaida mbele ya wenzetu ndani ya EA. Nawashauri wasomi wa Tanzania, thread za namna hii zinaonyesha kuwa bado tuna fikra zisizopevuka sawa sawa. Tuweka hapa thread zinazoweza kusaidia kupandisha elimu kwenye shule zetu na vyuo vyetu.