Vyakula vinavyoongeza Kinga ya mwili

Apr 26, 2016
23
28
Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku.

Hakuna dawa au chakula cha kula siku moja na kuponya tatizo la kushuka kinga ya mwili milele. Kinga ya mwili huongezeka ama kupungua kila siku kutegemea na umekula nini, umekunywa nini au hali ya ubongo wako kwa ujumla ipoje kwa siku hiyo, mathalani kama umeshinda una hasira hasira tu kutwa nzima lazima na kinga yako itapungua.

Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji DAWA YOYOTE. Ulivyo ni vile unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na dawa zako ziwe ni chakula unachokula. Kinga yako inapokuwa na nguvu na ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula 14 vinavyoweza kukusaidia

1. MTINDI
Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza kinga ya mwili wako.
moja.jpg

2. MATUNDA
Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

Unaweza kuamua pia moja ya mlo wako katika siku kama ni wa jioni au wa mchana au wa asubuhi uwe ni matunda tu na si kitu kingine zaidi. Jaza kwenye sahani yako ndizi, embe, papai, nanasi, tikiti maji, parachichi nk, sahani iwe na matunda tu kula hadi ushibe matunda tu.
mbili.jpg

3. Tui la Nazi
Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huwa na uwezo wa kuiimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali.

Matumizi ya nazi kama tiba kwa watu wenye UKIMWI duniani yalishika kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii. Waathirika wa UKIMWI toka sehemu mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba.

Dozi yake ni rahisi, kunywaji glasi nne za tui la nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na kupungua kwa kinga ya mwili na pia hung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama kinga yako imepunguwa basi anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu. Kama tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.
tatu.jpg

4. VITUNGUU SWAUMU
Hupatikana kwa wingi Tanzania! Japokuwa vitunguu swaumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

Chukuwa kitunguu swaumu kimoja, Kigawanyishe katika punje punje, Menya nusu yake (punje 8 au 10 hivi), Menya punje moja baada ya nyingine. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu, Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2.
nne.jpg

5. Mlonge
Maarufu kama mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji.

Karibu kila sehemu ya mti wa Mlonge inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Mlonge, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi kwa kuongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni.

Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;

Vitamini C – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.

Calcium (madini chuma) – Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara nne zaidi ya kile kinachopatikana kutoka kwenye maziwa.

Protini – Kirutubishi hiki ni mhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa.

Vitamini A – Kirutubishi hiki ni mhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.

Potassium – Kirutubishi hiki ni mhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya Mlonge ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi. Maua ya Mlonge yamejaliwa madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa na kuliwa kama mboga. Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Majani mabichi ya Mlonge ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia. Juisi ya majani ya Mlonge hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha. Pia juisi ya mlonge ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari. Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.

Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
tano.jpeg

6. Asali yenye mdalasini
Asali ni dawa kwa kila ugonjwa, zingatia tu unapata asali mbichi na nzuri ya asili kwani endapo utauziwa asali iliyochakachuliwa kuna hatari ya kuharibu afya yako zaidi. Katika kila lita moja ya asali ongeza vijiko vikubwa vya chakula 8 vya unga wa mdalasini na uchanganye vizuri kisha lamba kijiko kimoja cha chakula cha mchanganyiko huo kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja hivi kinga yako ya mwili itarudi katika hali yake nzuri.

7. UYOGA
Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!
saba.jpg

8. SUPU YA KUKU
Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

Mhimu ni kuwa supu hii ya kuku hakikisha ni ya kuku wa kienyeji tu.
nane.jpg

9. Ubuyu
Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku (kumbuka uwe ubuyu halisi). Ubuyu una vitamini C nyingi zaidi kuliko ile ipatikanayo kwenye machungwa au maembe.
tisa.jpg

10.VIAZI VITAMU(mbatata)
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu
kumi.jpg

11. KAROTI
Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!
11.jpg

12. SAMAKI
Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.
12.jpg

13. MATIKITI
Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.
13.jpg

14. MAJI YA KUNYWA
Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunwya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau glasi 8 hadi 10 za maji kwa siku ni muhimu kwa afya yako!.
14.jpg

Vitu vinavyoharibu na kushusha kinga ya mwili

1. Msongo wa mawazo (stress)
2. Vilevi vyote
3. Lishe duni (chakula kichache)
4. Kutokufanya mazoezi ya viungo
5. Kutumia dawa za kupunguza maumivu kila mara bila ushauri wa kitaalamu
 

Attachments

  • tatu.jpg
    tatu.jpg
    4.6 KB · Views: 339
Back
Top Bottom