Vurugu korogwe.!


Tunahitaji kutumia FORENSIC SCIENCE... Nchi Nzima

The best way ya kuwakamata hawa wezi wa sasa ni Forensic Science - badala ya kula pesa; ni kuapgrade POLICE
 
idumu chit chat....
maana kule tunapost mada iliyo kamili sio huku sihasa wanapost mada imevaa bukta....


hili jukwaa nalipenda, lanipa raha! kila mtu hupost chake, kwa muda wake. ni sawa na kule kwetu chi chat! kwi kwi kwi!
 
kwa hiyo wamemuua msamaria mwema aliyeenda kuripoti?
pamoja na kuwa polisi hawa-act mara tu tukio linaporipotiwa lakini haina maana kuwa bodaboda wachukue sheria mkononi...(na hili limekuwa ni tatizo kubwa ya hawa boda boda, kuchukua sheria mkononi....)

na mamlaka husika inajua tatizo hili imetulia tu sijui inaona raha au inafurahia.....

kwa ufupi...polisi na bodaboda ni janga la taifa....





 
huko korogwe kimenuka kweli
mtu moja wa bodaboda alichinjwa kama kuku,sasa waendesha bodaboda wakawa either wanawafahamu au wanawahisi waliofanya tukio,wakawakamata hao watu mchana peupe na kuwapiga visu baada ya kuwaua wakaanza kuwavuta na pikipiki hapo mjini wakiwa uchi wa mnyama na kwenda kuwachoma moto.gari za polisi toka tanga tanga zimeenda hapo korogwe.

kama unamtu unamfahamu hapo korogwe wewe mvutie tu waya
 
Dhambi ni lazima ikemewe,
Dhambi ikiachwa humgusa kila mtu,
Ubaya wa dhambi,
ni tabia yake ya kupatiliza,
huwaingiza waliokuwemo,
na wasio kuwemo.

Dhambi ya mtu mmoja,
ina uwezo wa kuangamiza taifa zima,
chuki ya mtu mmoja,
ina uwezo wa kuangamiza taifa zima,
Hasira ya mtu mmo in uwezo wa,
kuleta chuki taifa zima.

Ona dhabi ya rushwa,
inavyotufanya kwa nguvu kila siku,
tunadharirishwa katika nchi yetu.

Ona dhambi ya uongo ituangamizavyo,
uongo ni mtaji wa utajiri,
uongo ni dira ya taifa,
uongo una abudiwa na viongozi wetu?

ona dhambi ya wizi itutuavyo umasikini,
kuiba ni ujanja,
kuiba ni kuchngamka,
maaskofu wanaiba,
masheikh wanaiba,
rais anaiba,
mawaziri wanaiba,
Wengi wanatamani kuiba ili waukate.

ona dhambi ya uchoyo,
Magari 20 ya nini,
wakati barbara zenyewe hakuna?
mtu ana vimada 100,
lakini bado anatongoza wake za watu?
Unaiba pesa,
huwekezi popote,
unazificha Ulaya,
sasa uliiba za nini??
utazitumia lini?
Unamkataba na Mungu?

Dhambi,
inavyotafuna maendeleo yetu.

Ni lazima tukemee dhambi,
tena tukemee,
kwa nguvu na akili zetu zote,
au tuwe tayari kumwaga damu,
za wakosefu na wema pia.

Dhambi mkataba wake unasainiwa kwa damu.
 

Ni kweli kabisa Ruge Opinion, tunakoelekea ni kubaya sana sana.
Na serikali isipobadilisha mfumo wwake wa utawala, tutauana sanaa
 

Hapana aliyeuawa si msamalia mwema, ni mtuhumiwa baada ya msamalia mwema kwenda kuripoti na kuwezesha kuatikana mtuhumiwa.

Ni kwel kabisa pamoja na kwamba hawa ni waarifu but kifo kilivyowakuta kwa kweli ni humiliation ya hali yajuu. Maana waliburuzwa kama walivyozaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…