Matokeo ya Vpl katika viwanja mbalimbali leo tar. 16/09/2015.
Yanga 3-0 Prisons
Jkt Mgambo 0-2 Simba
Maji maji 1-0 Kagera suger
Mbeya city 3-0 Ruvu star
Stand United 0-2 Azam fc
Toto Africans 1-2 Mtibwa suger
Ndanda 1-0 Coast Union
Mwadui 2 - 0 African Sports
Leo ligi kuu ya Tanzania, VPL inaingia mzunguko wa pili. Yanga SC wanawakaribisha maafande wa prisons toka Mbeya. Ikumbukwe kuwa katika mechi yao ya awali, Prisons walitakata vilivyo licha ya kubanjuliwa magoli mawili kwa moja na Azam FC. Yanga nao waliwafundisha soka wateja wao Coast Union kwa kuwatandika mabao mawili kwa nunge na kujikita kileleni mwa ligi. Hivyo Tutarajie mtanange wa kasi uliosheheni ufundi mwingi na hivyo kutoa burudani Safi kwa mashabiki na wapenzi wa kabumbu. Karibuni
Natamani kuwaombea njaa kandambili ila naona ni dua la kuku, ni bora tu niwatakie ushindi nyambafuuu sina la kufanya.
Yanga ni CCM
Kama sikosei wewe ni mngoni wa pale Matalawe kama sio Mlilayoyo, huna tofauti na Nchimbi.Yanga ni CCM
Kwa jinsi alivyopambana na Azam leo Prisons ana kila sababu za kuibuka na ushindi tena wa kishindo. #Friends_Of_Prisons
Huyu jamaa namfahamu kuwa ni Mwana CCM, lakini pia nafahamu fika kuwa yeye si Mwana Yanga hivyo Yanga sio CCM.
Hivyo basi Deo Corleone wewe ni muongo!