Dua za kombe la mapinduzi na mechi ya ndanda zinaendelea kama kawaida. Wengine leo eti wanadanganya hakuna ibada, timu analosapoti likifungwa wanapotea humu wakiulizwa nilikuwa ibadani. Kaazi kwelikweli
Nimekipata kikosi kitakachoanza na kitakuwa kama ifuatavyo:
Manyika Peter.
Ramadhan Kessy
Mohamed Husein
Juuko Murshid
Hassan Isihaka ( C)
Jonas Mkude
Ramadhan Singano
Said Ndemla
Elias Maguli
Danny Sserukuma
Emanuel Okwi
Timu zinaingia uwanjani ili kuanza mtanange wa kukatana shoka, azam fc vs simba. kila la kheir lambalamba leo nipo kwenu kwa mkopo wa muda wa masaa mawili tu.
Leo mtani njoo kwetu tu, maana hata huku Azam tunaichukia balaa (siongelei wana-Simba wote)!!
Niwe mkweli, mi binafsi, yanga ikicheza na Azam, huwa najikuta nataka Azam ifungwe!! Sipendi kutaka Yanga ishinde, ila roho yangu inakuaga hivyo!