VODACOM , Wizi mtaacha lini?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,573
Reaction score
28,533
6Xxxxxxxxxx Imethibitisha. Imethibitisha. Tsh400,000.00 zimetumwa kwa 07xxxxxccc tarehe 8/8/19 saa 2:30 PM kwa ada ya Tsh8,500.00. Salio lako la M-Pesa ni Tsh250,771.80.tarehe 8/8/19 saa 2:30 PM kwa ada ya Tsh8,500.00. Salio lako la M-Pesa ni Tsh.....

.


Huo ndo ujumbe nimrpata toka VODACOM kwa kutumia huduma ya Mpesa.
Kutuma laki nne gharama yake 8,500!!!!
Huu ni wizi mchana kweupe.
VODACOM wataacha lini wizi.
 
Mkuu kwa maelezo yako inaonyesha hela umeituma moja kwa moja kutoka Vodacom kwenda mtandao washirika (mwingine) ambapo ada ya kutumia ni shs 1500 na ada ya kutolea 7000 zimeunganishwa pamoja na kuwa 8500, ambapo yeye uliyemtumia akienda kutoa hatokatwa tena hela, kwa maana nyingine ukitaka kutuma hela chagua kipengele kilichoandikwa mitandao mingine, tena utachagua aina ya mtandao husika wa unayemtumia ndipo utaandika namba yake , hapo utakuwa umekatwa ada husika (kama wewe hapo ni shs 1500) halafu uliyemtumia naye wakati wa kutoa atakatwa ada husika kulingana na kiasi ulichomtumia, hapo sina la zaidi, ahsante kwa kutumia mtandao wa Vodacom.
 
Kwan lazima hamia mtandao mwengone hiyo ni biashara unataka uwapangie ww gharama za kutuma izo pesa anzisha mtandao wako
 
Ufafanuzi mzuri mkuu.
Aongezee na hizo screen shot hapo chini.
Angalia sehemu za 400K kolam zote 2.
 
Voda kwangu hapana japo line IPO na huwa siwekagi line
 
 
Tutaacha kesho
 
Vifurshi ndio wanatembea nao balaa majamaa ni shida
 
Hata ikiwa voda kwa voda makato palepale
 
Ninachofahamu mkuu kwa kiasi hicho 8,500 ni makato kama umetuma kwa mteja asiyesajiliwa, kama angekuwa amesajiliwa kiasi ni Tzs 7,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…