Halmashauri ya Mui leo Imetengazaq kupitia ITV kwamba kuna viwanja vimeanza kutolewa.
Nimeona Tangazo lao inaonekana eneo ni zuri sana.
Jtatu kuna mtyu namtuma aende kuulizia maana bado sijapata Data kamili za namna ya uuzaji wao.
Tatizo la Halmashauriz etu ni kwamba wanatangaza viwanja halafu ukienda wanakuambia vimeisha,ukitoka hapo pembenei unakuta jamaa wanakuvuta wakuuzie tena.
Kuna sehem sipendi kuwataja humu,yaani walitoa Tangazo kwenye TV kama vile chemsha ----- ili mambo ya mauzo ya serikali yaonekane yamefuatwa kwa kutangaza kwenye vyombo vya habari.Lakini kwenda tu naambiwa vimeisha,ila nafika kituoa cha Daladala naona jamaa nyuma ananifuata na anadata zangu zote kama natafuta kiwanja.
Nikirudi Jtatu nitawapeni majibu,au kama watu mpo Kibaha basi nendeni Pale Halmashauri ili mtujuze zaidi