Viwanja kwa bei nafuu Morogoro

Tuwe makin jaman kuna maeneo kayataja yana utata. Kabla hujanunua hakikisha una taarifa zote mm nilitaka kuuziwa hifadhi huko
Duh! We labda ulienda nunua mikumi! Sa Mkundi kuna hifadhi ipi? Kama hauna uhakika mkuu acha kuropoka!
 
Basi unania mbaya mkuu....mimi mwenyeji maeneo hayo hata ukinitukana poa tu ila huko kuna wezi sana wa viwanja feki. kuweni makini tu jamani. Hapo mkundi/makunganya kuna hifadhi ya watu wa misitu ya taifa, ni eneo kubwa sana na wameng'oa mawe/vigingi/nguzo call whatever ili mgeni akienda asigundue. Hata hizo hati kuna watu wanazo hati feki pia. Kiujumla mnunuaji kuwa makini hayo maeneo kila mtu anayatolea macho....mm nikaamua kuhamia huku Iringa road japo hakuna umeme ila soon utafika tu na viwanja bado cheap sana...
 
Duh!mi moro nimetoka juzi tu huko.Kiwanja kihonda 8ml heka?mkundi laki 8????labda hiyo morogoro ya mwandiga kigoma.Watz kuweni makini.
 
mhhh mnatuchanganya sasa..plz tufafanulie mkuu sasa utajuaje hiki kiwanja fake..hii hati fake....utafumbua wengi macho
 

asante mkuu, huko Iringa rd bei zake zinaanzia ngapi? Unaweza niulizia? Umeme taratibu utafika tu
 
asante mkuu, huko Iringa rd bei zake zinaanzia ngapi? Unaweza niulizia? Umeme taratibu utafika tu

Kiwanja cha 2m au below ni eka nzima na kwa sasa msimu wa kulima unaingia bei zitazidi kushuka pia. Ila kwa mashamba hasa kwa mifugo bei laki 3 au chini/mapatano tu na muuzaji. Kuna jamaa jirani yangu ana eka mia (milima na mabonde) kwa 40m, ni pale sangasanga/njia panda mzumbe. Mimi sio dalali ila baada ya kutaka kulizwa mkundi/makunganya tena na viongozi wa serikali ya kijiji, nikakimbilia huku. Mimi sio dalali mm nina eka 14 na nataka kufuga tu
 
Vipimo ulivyoandika vinanichanganya. Unazungumzia ukubwa wa EKA MOJA au HEKTA MOJA.
 

Hayo mashamba ya laki8 ni kilometa ngapi kutoka msamvu?
 
Duh! We labda ulienda nunua mikumi! Sa Mkundi kuna hifadhi ipi? Kama hauna uhakika mkuu acha kuropoka!

Mkuu usibishe ipo hifadhi ya misitu ya taifa hayo maeneo (kati ya mkundi na huko kwa mwarabu), mimi mwenyewe ni mwenyeji mitaa hiyo ya makunganya. Nahisi wewe unataka kuwaingiza watu mkenge kwa kuuzia hifadhi!
 

Shilingi ngapi mkuu hapo iringa road
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…