<br />Ile kali zaidi ya Abunuwasi ni pale alipokuwa na shida na Sultani. Kufika mlangoni kwa sultani wale mlinzi akakataa kumruhusu aingie kumwona. Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa abunuwasi akiingia kwa sulatani atapata anachotaka maana alipendwa sana na sultani. Mkwara aliompa ni kwamba aahidi kuwa atakachopata kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi akakubali na akaingia kwa sultani. Kufika ndani sulatani anamuuliza sema shida yako abunuwasi maaana leo unaonyesha una huzuni. Abunawasi akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani akashangaa, kwa kosa gani? Abunuwasi akasema nichape tu Seyidina wangu na akasisitiza kuwa haondoki mpaka achapwe. Sulatani akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu sana viboko mia. Walipomchapa mpaka viboko hamsini Abunuwasi akasema vimetosha maana mlinzi wa pale getini tumekubaliana kuwa nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu yake kwa hiyo hivyo hamsini vilivyobaki atandikwe mlinzi. Sulatani kusikia hivyo akaghadhabika sana na kuamuru mlinzi aletew apigwe viboko hamsini tena vya uhakika. Mlinzi alijuta kuzaliwa, na hakurudia tena kuomba rushwa
Nakumbuka hivi vitabu viliwahi kupigwa marufuku Tanzania.
View attachment 37200
huyo elizabeti sio alikuwa ni mke wa Bulicheka?Abunuasi na mke wake Elizabeti
vitabu vile nitavipata wapi wana jf?hakuna website yenye hadithi zile?
vitabu vile nitavipata wapi wana jf?hakuna website yenye hadithi zile?
Abunuasi na mke wake Elizabeti
Kali nyingine ya Abunuwasi ni yule masikini aloyetowelea chakula chake na harufu nzuri ya samaki aliekuwa anapikwa nyumbani kwa tajiri. Kesho yake akakutana na yule tajiri na kuanza kumshukuru kuwa alifaidi sana chakula chake kwa harufu ya samaki kutoka nyumabni kwake.
Yule tajiri alisikitika sana na kukasirika kuwa ndio maaana samaki yule hakuwa na ladha sababu ya masikini yule kuvuta harufu yote ya samaki, hivyo alimwambia amlipe reale 5 kama fidia. Masik8ni yule fedha hiyom hakuwa nayo. Akaenda kushtaki kwa Sultan Harun Rashid ambaye naye alimkandamiza kuwa lazima alipe.
Mmasikini akaona aende kwa Abunuwasi kupata ushauri. Abunuwasi akamwambia yule masikini kuwa atamlipia deni hilo ila mbele ya Sultani. Siku ya kulipa Abunuwasi akaenda na hizo reale tano kwa sultani ili alipe deni hilo.
Wakati anataka kumpa yule anayedai abunuwasi akadondosha zile fedha sakafuni na kisha akamwabia yule tajiri kwa Chukua huo mlio kama malipo maana na yeye masikini alikula harufu tu.