Hali hiii kitaalamu inaitwa Exogenous ochronosis. Hii hali inasababishwa na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali inayojulikana kama Hydroquinone.
Tatizo hili linaweza kufifia taratibu baada ya Mtu husika anayetumia kuacha kutumia vipodozi vya namna hiyo, lakini kwa baadhi ya wagonjwa tatizo hili likishatokea ngozi yao haiwezi kurudia hali ya kawaida mpaka siku wanaingia kaburini.
Kwa ujumla wataalamu wanakataza matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hiyo ya Hydroquinone kutokana na madhara yake kwenye mwili ikiwemo mtu kutoa harufu kama shombo la samaki hali ambayo kwa kitaalamu inajulikana kama (Trimethylaminuria. )