Miss Neddy
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 14,684
- 8,760
Story za kuboroga nnazo telee maana ikiwa mtu kaboronga tunamchekaa siku ya pili anakua na ari mpya lol.....
Cousin yangu last year alipika kachori aliziunga vizuri sana tu sasa wakati wa kuchoma sasa ule uji kafanya mwepesi na mafuta hayajapata moto vizuri akazitia kachori kabla ya hapo nlikua namuambia umekosea hiki nkaambia nifunge bakuli langu, weeee kachori zilitumbuka zote akabaki kukaanga uji wenziwe walimchekajeee na mie mmoja wapo lol
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea
Yani mpaka nimejua kusonga ugali...nyumbani nishawalisha masotojo ya kila aina....mpaka leo nikitaka kusonga ugali bro wangu ananambia uji ukichemka nimuitee....hawaniamini....!
Ila siri ya ugali mzuri uji uchemkee uive na usiwe mwepesi sanaaa!
Tena mbona vizima vizima ndo vinanoga haswaaa. Naunga mkono kwa hili
hahhahahh...
mi siku ya.kwanza napika pilau I was 12,nliivisha wali vizuri then nkaeka pilau masala kwa juu nkaongeza na maji ya baridi nkakoroga na kuwasha jiko upya....hhehehe lilitokea bokoboko hataree lenye harufu ya pilau,ilibidi tule hvohvo kesho yake mama ndo akanifundisha kupika pilau
Niliwahi kupika wali nikajaza sufuria maji ili uchemke na kuiva vyema!!!! Kilichotokea ni matope halafu siku hio nikaachiwa nyumba, kidume nikaamua nijipikie chips nifaidi duh! Hadi leo nimeachana na biashara ya kupika naona sio fani yangu
Umenikumbusha na mi kuna siku nlipika wali ukawa bokoboko hatari.Mama alivofika mezani kufunua hotpot kabla hata hajaeka mdomoni akaniambia, siku nyingine nikipika ivo nieke kwenye thermos kabisa wajue ni uji wanakunywa.Nkikumbuka ayo maneno uwa nacheka.
Lol, uji wa mchele sio?
Mie nkipika chakula kama hakijakuja vizuri nanunaajee
cku nilipojaribu kupika egg chop, duuh ctasahau, c zikaanza kuachia ndani ya mafuta zikawa zinatawanyika tu, yaani nilicheka mpaka bac, cjajaribu tena!
Jaribu za ku bake
sku nyengine nlieka limau kachumbari ikawa chungu ka mwarobain. afu skuonja, hadi saa ya kula ndo kizaizai kikawa
Hahahahahahaha, umenichekesha sana.