Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 10,659
- 23,139
Hahahah hii ya dada angu
Siku tukatamani mchuzi wa nazi.....mie nikaandaa kila kitu yeye akakuna nazi mana yeye ndo mpishi siku hiyo saaa basi tui la nazi hilo lita 2 lol bibk jingi utasema linataka kupikiwa mchuzi wa shughuli lol nkamwambia abla (dada) hilo tui jingiiii sana weee akanishikisha adabu nkae kimyaaa....
Habibty ulipikwa mchuzi ma hotpot mawili kwa wingi nyama yengewe kilo 1 alafu mwepesiii kama wa maji hahahahahhahahaha nahiyo chumvi na ma ndimu acha tu ila huwezi amini nipishi hodari sana nowadays kwenye mapishi namugopajeeee......
Mkiona id Sherose jf chef ni yeye anakuja sopn
lol, huo unaitwa mbadalahahahahaha wapishi muna visaa....mi nikibugi simpelekei mtu pishi langu zaidi ya angyy. ...lol
ila hio mimambo ya kusahau kuweka hamira kwenye andazi au bp kwenye cake loh...sina hamu nayo...
Ramadhan moja nilikua mother house kabla sijaolewa na wazee hawakuepo hm kwahio mi ndo nilikua boss..lol, nikawaambia wanangu leo mukande andazi nikirudi job tunachoma..nimefikia kurudi tukakaaaaaa heee haliumuki nkaanza kumtafuta mkandaji (alikua ni mtu mzima fulani alikuja kututembelea akataka yy akande) ah nkashindwa kumwambia kitu nikabaki hivi ulikumbuka kuweka hamira ? Nae ni mbishi wee kanikazia macho nimeweka labda mbaya tu...lol ikabidi niyachanganye tena upyaa na ilikua late badala ya andazi nikamua kusukuma km chapati..tukala chapati za sukari...mh
Habari zenu wanajiko.
Leo ningependa tushee mambo yanayotutokea jikoni, yale ya vituko vituko.
Mie mengi yamewahi kunikuta lkn ntaweka machache tu.
Kuna siku mama yangu aliniwachia niangalie pishi la mseto, sikujua kama kabla haujaepuliwa haukorogwi na mwiko si niukoroge, wacha mseto uungue. Nligombwajeee mpk leo nimejua kama mseto haukorogwi hadi uepuliwe ndo usongwe kama ugali.
Nlikua nkikaa jikoni na mama kupika, pishi kama halijaja vizuri basi hufukuzwa jikoni ati naambiwa macho yangu ndo yameharibu, lol.
Kuna siku nlikuwa nataka kukaanga chips, nkakosea kwenye karai badala ya kuweka mafuta nkaweka siki, si muda jikoni kumejaa moshi na harufu ya ajabu kuja kuangalia kumbe nimebeba chupa ya siki badala ya mafuta.
Usiombe kuumua maandazi ukaweka sukari nyingi, utalala hata siku mbili hayajaumuka, hii mpk leo hii mi mwenzenu mara hubugi step.
Haya wana jiko hem na wengine waeleze vituko vinavowapata jikoni, au vilowahi kuwapata wakati wanjifundisha kupika, au kitu gani hupendi uwapo jikoni.
naamini makofi hayo mawili ndio yaliyokufanya hadi hii leo ukawa mpishi mzuriHabibty hahahahah mie hiyo ya maandazi ilowahi nikuta zaman siku mama kaenda shopping kwa ajili ya eid ilikua ramadhan nakumbuka basi akaniambia nipike maandazi yeye akirudi atakuja kuchoma....shoga nkalikanda andaaz lainiii wakat anaraudi sasa karibia maghrib anataka kuyachoma bado hayajaumuka na mie kila nkiyasubiri hayaumuki weee kumbe mesahau kutia hamira nlisemwa na makofi mawili mazuriiii lol
ha ha haaaa, inaelekea ushatupa vingi wewePindi najifunza kupika Ugali, si nikapika mbichi, manake niliweka unga hata maji hayajachemka. We nilichokifanya ni kutupa batini kabla mtu hajaona Halafu nikaanza upya!!
umeona enhee? labda wanaona haya kuchekwaJameni hivyo vituko jikoni ni kwa kina dada pekee. mbona sie kina kaka na baba tupo kimya, inamaana sie hatujui kupika ama ndio ladies first.
lol, mwanzo mgumu. lakini tuseme haya na yale kwenye kupika kadri ukikosea ndo unazidi kujua zaidi kupika. ila kuna watu wakikosea mara moja tu wanakata tamaa hawarudii tena kupika kile kituumenikumbusha mbali nikiwa binti mdogo ndio najifunza kupika, mama alitoka akaniachia pishi la wali na kukaanga mchuzi wa nyama. Nikatia mafuta jikoni, moto mkali mie nakata vitunguu kidogo dogo. Kuja kuvitia jikoni, moto si ukawaka sufuriani, kwa woga acha nimwage kila kitu, mafuta yalikuwa ndo yale yale, so ikabidi nitie vitunguu, nyanya na maji kwenye nyama nikachemsha. piga picha ya nyama ambayo haijanona, mchuzi maji matupu. Huo wali sasa - waswahili wanaita madida (wali ambao haujakauka vizuri). Aliporud, saa ya makulaji acha nigombezwe. ila baba alinisifia eti kwa vile chakula kiliiva na kililika. Sisahau hiyo stori.
lol, mwanzo mgumu. lakini tuseme haya na yale kwenye kupika kadri ukikosea ndo unazidi kujua zaidi kupika. ila kuna watu wakikosea mara moja tu wanakata tamaa hawarudii tena kupika kile kitu