Vitambulisho vya uraia

Zamaulid

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2009
Posts
19,955
Reaction score
16,006
Hivi vitambulisho vya uraia ni kwa ajili ya kusajilia line za simu tu? Mbona msisitizo umekuwa kutumia vitambulisho hivyo kusajili line za simu tu?

Nielewesheni matumizi ya vitambulisho hivyo.

Sio kila kiuzwacho sokoni chafaa kununuliwa.
 
Hivi vitambulisho vya uraia ni kwa ajili ya kusajilia line za simu tu?!mbona msisitizo umekuwa kutumia vitambulisho hivyo kusajili line za simu tu?

Nielewesheni matumizi ya vitambulisho hivyo

Siyo Kila Kiuzwacho Sokoni Chafaa Kununuliwa
Ngoja waje

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Vitasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali
2. Vitasaidia kumtambua mhusika kirahisi anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.
3. Vitarahisisha kuwatambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye benki na asasi mbalimbali za fedha nchini.
4. Vitasaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari la kumbukumbu la kielektroniki.
5. Vitawezesha kumtambua mtu anapofanya biashara au shughuli nyengine kwa kutumia majina tofauti.
6. Vitafanikisha kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii. Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia wa Tanzania anastahili kupata kirahisi kwani kupitia kitambulisho mtu atatambulika kirahisi(nani ni nani?, yuko wapi?, na anafanya nini? katika taifa hili.
7. Vitasaidia kuondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ‘payroll’ ya Serikali.
8. Vitaimarisha utendaji kazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostahafu.
9. Vitarahisisha zoezi la kuhesabu watu (sensa).
10. Vitarahisisha zoezi la kuhuisha daftari la wapiga kura, ambapo kwa sasa hufanyika mara mbili kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Kama ni kwa niaba ya laini tu wengi watasajili kwa vitambulisho vya wengine.
 
Hivi kila mtu ameshapata kitambulisho chake?Mbona purukushani ya kuvitafuta imepungua
 
Mi nimepata cha kwangu, kama vipi njoo nikusajilie jirani


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Huyu jimena nilimuonaga miaka ya nyuma kabla sijawa mwanachama wa jf. Hivyo kwa kuwa nimemwona Leo nikiwa mwanachama nimeamua tu kum quote ili nitimize ndoto ya Ku quote MTU niliyemwona zamani jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…