Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Naamini katika kila dini kuna watu wafuasi wa kweli wa Mungu ambao kwao uonevu haupiti bila hukemewa.tatizo ni kuwa ccm imewanunua baadhi ya viungozi wa dini moja , hivyo wakisimama viungozi wa dini ya kikristo kukemea maovu ya watawala, haraka haraka watajibiwa na baadhi ya viongozi wa kiislamu, viongozi hawa wamejipa kazi ya kuwa wasemaji wa ccm na serikali yake. Na sababu wanayotoa ni kuwa viongozi wa kikristo wanaiandama serikali kwa sababun rais ni muislamu.mtego huu uliotegwa na mafisadi umewanasa baadhi ya viongozi wa kiislamu hivyo kufanya kazi ya ukombozi wa taifa letu toka kwa wakoloni weusi kuwa ngumu.na huu ni ubunifu wa jk wagawe uwatawale milele.
Nina maana kuwa kati ya makundi yote ya dini sio wote wanaoweza kununuliwa. Penye ukweli uongo hujitenga.Kwahiyo unakubaliana na "matamko ya viongozi wa Kiislam na Kikristo"
If that is the case then good move.
Viongozi wa kisiasa wamejaribu kila wawezalo kuwanyamazisha viongozi wa dini hasa pale wanapokemea au kukosoa vitendo vya kidhalimu. Mara wamesemakana kuanzisha udini na kadhalika. Mara nyingi wameshauriwa kutokuonyesha kuegemea upande wowote. Lakini wakati kuna uonevu wa lolote au kuna lolote lisilo haki kwamba linatendwa na viongozi wa serikali au vyama vya siasa basi ni wajibu wa viongozi wa dini kusimamia misingi ya haki bila kujali mkosaji ni nani?
Dr. Desmond Tutu aliwahi kusema hivi.
"If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality."
Archbishop Desmond Tutu.
TAFSIRI ISIYO RASMI:
Kama ukisema huna upande katika uonevu, basi umechagua upande wa muoneaji. Kama tembo ataweka mguu wake juu ya mkia wa panya halafu wewe ukasema hauna upande , basi panya hatafurahia kutokuwa kwako na upande.
Nawasilisha kwenu viongozi wa dini na wale wote mnaowalaumu kwa kukemee uonevu.
Kwahiyo unakubaliana na "matamko ya viongozi wa Kiislam na Kikristo"
If that is the case then good move.
Kila nchi inaustaarabu na tamaduni zake, leo hii usa kwenyewe kuwa muislam ni issue kuwa rais, england kanisa ni sehemu ya uongozi.
Maana yangu ni kuwa kwakuwa tutu katamka ya kisiasa nchini kwake hayo ni mazingira ya kwao kama ilivyokuwa ngumu kuingiza utawaa na kanisa hapa bongo kama uk, au tuwe kama usa au iran nk
Ni wajibu wa watu kujua mazingira na misingi iliyotumika kutufikisha, hapa tulipo.
Leo hii hatuwezi kuruhusu viongozi wa dini kuwa mahakimu wetu wa kuanza na kugeuka kuwa kama masignatory wanao endorse huyu si meya halali hatumtambui kesho watesema huyu si mbunge halali hatumtambui, wao ni kina nani?
Kwani dini ni nini, ni wangapi wanaamini hayo mapokeo ya dini na kudhani ndio sahihi kwa kuokoa jamii, kama dini zenyewe ndio hizi za kukatana mikono na kuua wanaokuwa against na wewe hata kwa kuchinja, kama dini zenyewe ndio hizi za kuwalawiti watoto wadogo na kuleta mafunfisho ya wizi wizi na kutapeli watu kwa majina matamu ya nabii,mtume,askofu nk, basi nasema wewe umepotoka
Viongozi wa dini wanajukwaa lao la kusafisha waumini wao madhabahuni kama wameshindwa huko wasikimbilie ktk siasa.
Leo hii kanisa rwanda ni sehemu kubwa wa yaliyotokea na kisingizio ilikua ni kujifanya dini haiwezi kukaa kimya katika mambo ya siasa.
Tafakari kwa kina utapatamajibu
Mnatoka nje na mada. Suala kuu hapa ni kupiga kelele pale ambapo tunaona uonevu. Viongozi wa dini ni mfano unaotumika kwa watu wa nje na siasa lakini walio viongozi kuwatia moyo kupiga kelele kwa uonevu. Haijalishi kelele inapigwa na nani. Kama ni kelele ya haki kila mtu ataiunga mkono. Hapa tuna maana kuwa hata kama ni mashirika yasiyo ya serikali au wanaharakati wanapaswa wapige kelele.Mkuu mimi ni mkristo, lakini hapo umeuliza swali lenye manti nzito sana kwa mtu muelewa, je tukubaliane na matamko ya dini na madhehebu yote? maana isie onakana matamko fulani tu ndio sahihi, mind that kunamadhebu kama ya akina kibwetere nao ni dini.
I real hate this shit kuchanganya siasa na dini
Suala hapa sio kuhubiri dini au siasa. Suala alilosema Tutu halihitajii kuwa katika eneo fulani la kijiografia ili uone ukweli huo. Huwa hakuna ukweli wa eneo fulani na eneo jingine. Hapa anachosema ni kuwa ukiona uonevu kisha ukaunyamazia basi unakubaliana na huo uonevu na pia ukiona mtu anaonewa na husemi chochote, basi yule anayeonewa hawezi kufurahia kuwepo kwako au kushuhudia kwako. Kuhusu viongozi wa dini kutokuzungumzia maslahi ya nchi yao kwa kisingizio cha kuwa wahubiri wa dini liliwahi kujibiwa.
Jibu lilikuwa " Endapo wote tunasafiri katika boti na mara mmoja wetu akaaza kutoboa boti, kisha msafiri mmoja ambaye sio nahodha akapiga kelele, Acha Acha, kisha anayetoboa anasema It's none of your business, ( Haikuhusu nyamaza).
Je utanyamaza kwa kuwa anakuambia nyamaza? Yaliyotokea Rwanda yalisababishwa na viongozi wa dini waliounga mkono matendo ya uonevu na yasiyo ya haki kama ambavyo hapa Tanzania wako wanaounga mkono viongozi wa kisiasa kwa kila wanachofanya hata pale ambapo ni UONEVU WA WAZI. Uonevu huchochea kuondoka kwa amani. Amani huzaliwa kwa matendo ya haki. Haki ikiondolewa
AMANI INAKUWA IKICHEZEWA.
Mnatoka nje na mada. Suala kuu hapa ni kupiga kelele pale ambapo tunaona uonevu. Viongozi wa dini ni mfano unaotumika kwa watu wa nje na siasa lakini walio viongozi kuwatia moyo kupiga kelele kwa uonevu. Haijalishi kelele inapigwa na nani. Kama ni kelele ya haki kila mtu ataiunga mkono. Hapa tuna maana kuwa hata kama ni mashirika yasiyo ya serikali au wanaharakati wanapaswa wapige kelele.
Iko kama Tropical na Paulss ni ndugu waliokuwa pamoja au ni yuleyule?
Mkuu sawa unaposema kupiga kelele viongozi wa dini je tufate kelele za maaskofu wa arusha au tufuata za waislamu wa karmjee?.
Huitaji akili ya ziada kujua hatari iliopo kuruhusu malumbano kama haya unayoyaita kelele za haki