Report ya IMF inasema kwamba, uchumi wa Urusi umefanya vizuri tofauti na ilivyotegemewa.Kupanda mchongoma Kushuka ndio Ngoma. Wachinjaji walienda Machinjioni kuchinja Ngombe walipo fika wakakuta Ngombe wameshika Visu na Kuwasubiri wachinjaji.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha YALE nchini Marekani wanasema uchumi wa Urusi unakabiliwa na uharibu mkubwa kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi, licha ya Moscow kupuuzia athari hizo.
Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa kazi yao inatilia mashaka madai ya Moscow kuwa uchumi wake bado uko imara na kuwa nchi za Magharibi zinaumia Zaidi kupitia kile kinatajiwa kuwa ni "vita vya kuzorota uchumi.”
Utafiti huo wasemaje?
Timu ya watalaamu wa Yale ilitumia data ya watumiaji bidhaa na takwimu kutoka washirika wa kimataifa wa kibiashara na usafirishaji bidhaa wa Urusi, kupima shughuli za kiuchumi miezi mitano baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini UKRAINE [emoji1255]
Waligundua kuwa msimamo wa Urusi kama muuzaji wa bidhaa ng'ambo umeyeyushwa kabisa, baada ya kulazimika kugeuka kutoka kwa masoko yake makuu barani Ulaya kuelekea Asia..
Utafiti huo unasema uingizaji wa bidhaa nchini Urusi umeporomoka tangu vita vilipoanza, na nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa za kununua pembejeo, vipuri na teknolojia.
Timu hiyo iligundua kuwa uzalishaji wa ndani wa Urusi umekwama kabisa na haina uwezo wa kujaza nafasi za biashara zilizoanguka. Watayarishaji wa ripoti hiyo wanasema hali hiyo imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa na hasira ya watumiaji.
Nchi zaMagharibi zimeiwekea Urusi vikwazo. Huku kukiwa na karibu kampuni 1,000 za kimataifa zilizofunga milango yao nchini humo, Urusi imepoteza kampuni ambazo zinawakilisha karibu asilimia 40 ya patojumla la ndani kwa mujibu wa utafiti huo.
Ripoti hiyo imesema Putin anaingilia kati kwa kutumia njia isiyo endelevu ya kifedha ili kuficha mapungufu ya muundo wa kiuchumi.
Iliongeza kuwa bajeti ya serikali ya Urusi imetumbukia katika nakisi kwa mara ya kwanza na fedha za Kremlin zipo katika hali ngumu mno kuliko inavyoeleweka kawaida.
Wakati huo huo, watafiti hao wamesema masoko ya kifedha ya Urusi – wakiweka jicho kwa utabiri wa usoni – ndio yanayofanya vibaya Zaidi ulimwenguni, hali inayopunguza uwezo wa kuvutia uwekezaji mpya wa kuufufua uchumi.
"Tangu uvamizi huo, takwimu za kiuchumi za Kremil zimekuwa za kuchaguliwa, kwa kutoa maeneo ambayo hayaonekana kuwa mazuri kwao na kuchapisha tu yanayowafaa” unasema utafiti huo.
Urusi imewekewa vikwazo vya mafuta
Takwimu mpya za uzalishaji wa viwanda wa Urusi kwa mwezi Juni zinaonyesha kuwa iliathirika pakubwa katika sekta nyingi ikilinganishwa na mwaka jana. Kwa magari, uzalishaji ulipungua kwa asilimia 89 wakati kwa nyaya za mawasiliano ulishuka kwa karibu asilimia 80. Nini kinachofuata kwa uchumi wa Urusi?
Waandishi wa utafiti wa Yale walisema Urusi haina mbinu ya kujiondoa katika janga hilo la kiuchumi kama washirika wa Magharibi wataendelea kuungana kuhusu vikwazo.
Utafiti tofauti wa Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa na Usalama uliochapishwa Juni pia unaashiria kuwa uchumi wa Urusi upo kwenye misukosuko mingi, licha ya kustahimili siki za mwanzo za kutangazwa vikwazo.
"Athari za vikwazo ndio zimeanza tu kushuhudiwa: matatizo ya uzalishaji na usambazaji yanaongezeka na mahitaji yanapungua kwa kasi.” "katika kipindi kirefu, uchumi wa Urusi utadorora Zaidi wakati kwa kiasi fulani ukiachana na biashara ya kimataifa.” Ilisema ripoti hiyo.
Source DW. Aljazeera
=========
NB: Russia kuomba msaaada wa kijeshi IRAN ni ishara tosha.
by the way tutauamini huu utafiti hadi tutakapo pata utafiti mbadala toka russia [emoji635]
Kumbe na wewe mdau wa Gravitas kama mimi mwanadada Parki ananikosha sana
Sio inasemekana. Taarifa za ndani ya Urusi data muda fulani mwezi huu mwanzoni zilionesha uzalishaji wa magari umeshuka kwa 86%, wiki hii kuna data zao zilionesha uzalishaji umeshuka kwa zaidi ya 90% ila chanzo cha ndani ya Urusi kilichoandika sijui credibility yake na sikuona data walizipataje.Inasemekana imepungua kwa zaidi ya 80% huo utengenezaji wa magari.
Hii ya ruble kupanda dhidi ya dollar waliizungumza mno kipindi cha mwezi wa tatu hivi.
Report ya IMF ya lini. Uchumi wa Urusi hauaminiki kwa wawekezaji, ukishaona sarafu ya nchi inapanda thamani 20% within 2 months na kushuka 20% within 2 months ujue hakuna kampuni serious itaenda kule.Report ya IMF inasema kwamba, uchumi wa Urusi umefanya vizuri tofauti na ilivyotegemewa.
Uchumi wa marekani ndio unapata tabu makampuni yamepoteza billions kwasababu ya kushuka wa dola.
Kweli bhaana, jamaa wameenda mpaka Uganda, kweli huko hapakaliki. Nahisi mpaka sasa viongozi na wale vibopa wa Russia wanakamua fedha zao mfukoni badala ya hazina ya Taifa. Hawawezi gusa hazina ya Taifa sababu wanajua watauporomosha uchumi kwa kasi sana.Russia anatafuta ushirika na nchi kama Uganda [emoji848] hii Hali inafikirisha sana , maana urusi Kwa kipindi kirefu hanaga mda na mataifa ya Africa.., wanaweza kutuficha takwimu, lakini matendo yenyewe ni ushindi tosha
Hii france 24 habari ya siku 5 zilizopita, utaipata hata sources nyngne Russia doing better than expected despite sanctions: IMFReport ya IMF ya lini. Uchumi wa Urusi hauaminiki kwa wawekezaji, ukishaona sarafu ya nchi inapanda thamani 20% within 2 months na kushuka 20% within 2 months ujue hakuna kampuni serious itaenda kule.
Marekani hata ufanyeje, huwezi fanya USD ikue kwa asilimia zote hizo. Iko stable hata ulete vitisho gani, uchumi wa Marekani hauna tishio walau kufikia lililokuwepo 2020 kwenye peak ya COVID-19
France24 wanasema uchumi wa Russia unahimili vikwazo na kufanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa. Hiyo ni kweli kwa mtu yeyote mwenye akili wahusika wa uchumi nchini Urusi wamefanya kazi nzuri sana.Hii france 24 habari ya siku 5 zilizopita, utaipata hata sources nyngne Russia doing better than expected despite sanctions: IMF
Lakini Bwana Jo huko US watu hawamwelewi uchumi na inflation imewachanganyaFrance24 wanasema uchumi wa Russia unahimili vikwazo na kufanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa. Hiyo ni kweli kwa mtu yeyote mwenye akili wahusika wa uchumi nchini Urusi wamefanya kazi nzuri sana.
IMF imetabiri uchumi kukua kwa 2.5% mwaka huu ila bado kuna contraction ya 6%. Generally hakuna performance nzuri ya ukuaji, ila kupambana na vikwazo wahusika wanastahili tuzo
Hakuna first world country yeyote ambayo wananchi hawalalamiki, they are too much demanding. Mfano kichomuondoa Waziri Mkuu wa Italy ni nini hasa, kinachomuondoa Boris Johson pale UK ni kufanya party kipindi cha COVID-19 wakati kuna sanctions. Sababu ambazo ungekuwa Russia ukazisema unafariki bahati mbaya baada ya kuteleza na kudondoka kutoka dirisha la apartment yako huku mkeo akifariki bahati mbaya hapohapo baada ya kujikabaLakini Bwana Jo huko US watu hawamwelewi uchumi na inflation imewachanganya
Kwa hiyo wewe umeona wa kuwaamini ni Wamarekani waliosema Saddam ana silaha za maangamizi...wakakuta hewa tu??
France24 wanasema uchumi wa Russia unahimili vikwazo na kufanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa. Hiyo ni kweli kwa mtu yeyote mwenye akili wahusika wa uchumi nchini Urusi wamefanya kazi nzuri sana.
IMF imetabiri uchumi kukua kwa 2.5% mwaka huu ila bado kuna contraction ya 6%. Generally hakuna performance nzuri ya ukuaji, ila kupambana na vikwazo wahusika wanastahili tuzo
Bwana Ewura mbona hueleweki... Huko juu umedai uchumi wa Russia ni mmbaya mno na hakuna kinachoeleweka hapo juu umekuja na hilo la kuwasifia wachumi wa Russia kwa kazi nzuri,. Swali je hizo sifa unazotaka wapewe hao wachumi za kazi nzuri ipi!!!?? Kwa kuufanya uchumi uwe imara au kwa kuudondosha!!!!!????France24 wanasema uchumi wa Russia unahimili vikwazo na kufanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa. Hiyo ni kweli kwa mtu yeyote mwenye akili wahusika wa uchumi nchini Urusi wamefanya kazi nzuri sana.
IMF imetabiri uchumi kukua kwa 2.5% mwaka huu ila bado kuna contraction ya 6%. Generally hakuna performance nzuri ya ukuaji, ila kupambana na vikwazo wahusika wanastahili tuzo
Kuhimili vikwazo tofauti na ilivyotarajiwa na kufanya vizuri kiuchumi hujui tofauti yake? Unashindwa kuelewa context nyepesi.Bwana Ewura mbona hueleweki... Huko juu umedai uchumi wa Russia ni mmbaya mno na hakuna kinachoeleweka hapo juu umekuja na hilo la kuwasifia wachumi wa Russia kwa kazi nzuri,. Swali je hizo sifa unazotaka wapewe hao wachumi za kazi nzuri ipi!!!?? Kwa kuufanya uchumi uwe imara au kwa kuudondosha!!!!!????
Soma hiyo link aliyotoasource ya hizi data pls
Uchumi WA Rusia utayumba lakini hautaporomoka kama west walivyotarajia Kwa vikwazo walivyowekewa Rusia ulaya na Marekani walijua Kuwa Rusia hii vita hata kwenda nayo miezi ata mitatu haitafika ata Rudi nyuma ili kulinda uchumi wake Ila matarajio yamekuwa tofautii na Hali ikiendelea ivi kuna hatihati wakalamba matapishi Yao Kwa kuondoa vikwazo walivyoweka wao wenyewe hasa upande WA gesi, mafuta, mbolea,chakula, makaa ya mawe na vipuri hatari za kiuchumi mbeleni ni kubwa snaa Kwa ulaya kuliko Rusia utulivu WA Rusia kwenye kushughulikia ivi vikwazo limekuwa Jambo la faida sana kwao hawakurupuki wanafanya kama hawatakiKuhimili vikwazo tofauti na ilivyotarajiwa na kufanya vizuri kiuchumi hujui tofauti yake? Unashindwa kuelewa context nyepesi.
Ukiwa mahututi ukawekewa hadi mashine ya kupumua, ukakaa wiki mbili ukipambana. Mtu akisema una afya nzuri atakuwa na akili sawasawa? Mtu akisema unaendelea vizuri tofauti na ulivyokuwa na hali mbaya na walivyoogopa kukupoteza hapo haieleweki anamaanisha nini?
Bado naiona CIA fikra zake zipo sawasawa, Russia atavumilia hii hali kwa muda tu. Utafika wakati hatoweza kuvumilia, kuna muda atasitisha ama kupunguza kabisa vita yake huko Ukraine.Uchumi WA Rusia utayumba lakini hautaporomoka kama west walivyotarajia Kwa vikwazo walivyowekewa Rusia ulaya na Marekani walijua Kuwa Rusia hii vita hata kwenda nayo miezi ata mitatu haitafika ata Rudi nyuma ili kulinda uchumi wake Ila matarajio yamekuwa tofautii na Hali ikiendelea ivi kuna hatihati wakalamba matapishi Yao Kwa kuondoa vikwazo walivyoweka wao wenyewe hasa upande WA gesi, mafuta, mbolea,chakula, makaa ya mawe na vipuri hatari za kiuchumi mbeleni ni kubwa snaa Kwa ulaya kuliko Rusia utulivu WA Rusia kwenye kushughulikia ivi vikwazo limekuwa Jambo la faida sana kwao hawakurupuki wanafanya kama hawataki
Ulaya walikuwa wanaiona Rusia kama nchi ambayo walikuwa hawahiitaji kwenye uchumi wao Ila Kwa yanayotokea saivi kwenye chumi zao naisi ni ngumu kuitenganisha ulaya na Rusia
Wanasoma biblia na kuvaa misalaba kwanini wasiwe wateule, ninachowapendea Russia hawavai makobazi wala hawafugi majini.
Malengo yake yakifikiwa wala hatajiweka kwenye hii vita sana akikamilisha eneo ya donesk kulimiliki atapunguza hii operations Kwa asilimia kubwa naona vita kubwa ikienda kupiganwa pale Odessa na inaweza kuchukua ata miezi miwili kama wakiimiliki basi itabaki kuzuia mashambulizi ya Ukrein wengi wanaichukulia Rusia kama pilipili hoho Ila bado ana uchumi imara pamoja na vikwazo vyote walivyopigwaBado naiona CIA fikra zake zipo sawasawa, Russia atavumilia hii hali kwa muda tu. Utafika wakati hatoweza kuvumilia, kuna muda atasitisha ama kupunguza kabisa vita yake huko Ukraine.
Wacha na mimi nitie neno hapo mkuu, Vikwazo vya kiuchumi vina mbio mbili.Utafika wakati tutaanza kuuona moshi, hapo ndipo tutaona moto unaofukuta chini ktk nchi ya Urusi. Ukiondoa ushabiki, kwa vikwazo vya Russia, hawezi kubaki salama kiuchumi.
Na atakuwa anapita ktk hali ngumu mno, tusisahau kuwa fedha za wafanyabiashara wa Urusi, mali zao n.k ambazo vipo Ulaya na America, vyote vimepigwa pini.