Vikwazo vya marekani kwa iran vyafeli kwa asilimia 99% Iran na Ulaya kufungua kanali maalum ya mabadilishano ya fedha kibiashara

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Trump azidi kupata pigo; Iran na Ulaya kufungua kanali maalumu ya mabadilishano ya fedha za kigeni
Siasa za Marekani za kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimezidi kupata pigo baada ya nchi za Ulaya na Tehran kuamua kufungua kanali maalumu ya kifedha kwa ajili ya wasafirishaji nje bidhaa wa pande hizi mbili.
Gavana wa Benki Kuu ya Iran, Abdolnaser Hemmati ametangaza habari hiyo na kuandika katika moja ya kurasa za mitandao ya kijamii kwamba, licha ya Donald Trump kuitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran ili kukwamisha mabadilisho ya kibiashara baina ya Tehran na nchi za Ulaya, lakini nchi hizo haziko tayari kufuata siasa hizo za Trump na zimeamua kufungua kanali mpya ya mabadilisho ya fedha ili kurahisisha miamala ya kiuchumi na kifedha baina ya pande mbili.
Gavana wa Benki Kuu ya Iran ameongeza kuwa, kanali hiyo ya kifedha ya Iran na Ulaya itaruhusu wafanyabiashara wa pande mbili kupata fedha zao za kigeni na vile vile hiyo itakuwa ni aina fulani ya mkataba wa kifedha baina ya Tehran na Umoja wa Ulaya.
Amesema, kikao cha wiki iliyopita cha Umoja wa Ulaya kilichofanyika mjini Brussels Ubelgiji kilijadili suala hilo.
Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Mei 2018, Donald Trump alitangaza kuitoa Marekani kwenye mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA yaliyofikiwa baina ya Iran na kundi la 5+1 mwaka 2015 na alitishia kuyawekea vikwazo na kuyakwamisha mashirika yote yatakayofanya kazi na Iran hata kama si ya Marekani.


KWA KINGEREZA:-

Details of payment channel to be released in near future

Governor of Central Bank of Iran (CBI) Abdolnaser Hemmati
Iran and European signatories of the Iran nuclear deal, officially known as the Joint Comprehensive Plan of Action (JCPOA), will establish a special payment channel in the near future, Governor of Central Bank of Iran (CBI) Abdolnaser Hemmati said.
Hemmati said the channel will serve as a monetary agreement between Iran and Europe and added the two sides discussed the details of the channel in a meeting held last week in Brussels.
“The channel is to be established based on a common understanding that the Iranian and European businesses are eager to maintain their ties despite the US sanctions,” he noted.
Iran and Europe, Hemmati added, decided to establish a special payment channel to facilitate the transactions between their businesses. “Through the channel, the two sides’ exporters can obtain their foreign exchange income,” he said.
The governor said Iran and Europe want to make operational the channel as soon as possible, adding, the details of the financial mechanism will be released in the near future.
The channel was first presented in a ministerial meeting between Iran and European signatories of the JCPOA held in New York in September.
US President Donald Trump announced in May that Washington was pulling out of the Iran nuclear deal which lifted nuclear-related sanctions against Tehran in exchange for restrictions on Tehran's nuclear program.
 
We jamaa wewe! Una "roho ya paka" linapokuja suala la Iran. Hebu mcheki jamaa yako anavyouza mapipa ya mwisho mwisho kwa mchina kabla ya shughuli yenyewe hapo Nov. 04; China yasitisha ununuzi wa mafuta ya Iran kuhofia vikwazo toka Marekani - JamiiForums
shughuli ipo wapi hapo november 4 wakati ulaya na iran ni biashara kama kawaida?Hahahaha halafu Vikwazo vya kipuuzi vya donald trump vimefeli, angalia nchi kama india uturuki, latin america na china bila kuisahau urusi wanaendeleza biashara na iran, Hivyo vikwazo vimegeuka mwiba kwa wamarekani wenyewe, halafu kuhusu kwamba eti china imestop kununua mafuta kutoka iran hizo ni ngano za washngton tu, China haiwezi kuacha kununua mafuta iran kamwe,
Eti china aache mafuta ya iran kisa mashinikizo ya washngton hahahahaha hizi ngano huwa mnaziota saa ngapi?hahahaha
 
shughuli ipo wapi hapo november 4 wakati ulaya na iran ni biashara kama kawaida?Hahahaha halafu Vikwazo vya kipuuzi vya donald trump vimefeli, angalia nchi kama india uturuki, latin america na china bila kuisahau urusi wanaendeleza biashara na iran, Hivyo vikwazo vimegeuka mwiba kwa wamarekani wenyewe, halafu kuhusu kwamba eti china imestop kununua mafuta kutoka iran hizo ni ngano za washngton tu, China haiwezi kuacha kununua mafuta iran kamwe,
Eti china aache mafuta ya iran kisa mashinikizo ya washngton hahahahaha hizi ngano huwa mnaziota saa ngapi?hahahaha

sasa mbona wajichekesha chekesha tu,kulikoni mkuu???
 
Acha uongo wewe.
Hatua iliyofikiwa mpaka kwa vikwazo vya kiuchumi kwa Iran ni majadiliano ya ama kuzima SWIFT services au la, au kuangalia namna bora ya SWIFT kumonitor transactions za Iran zilizolengwa kuzuiwa. Na haya majadiliano yanahusisha mataifa karibia yote ya Ulaya.

subiri ifike tarehe nne ndio utaelewa
 
Tukumbuke, maelekezo ya Trump ni kwamba, ikifika tarehe 4 Nov, hakuna kununua hata tone la mafuta kutoka Iran.
MAFANIKIO.
1. Bei ya mafuta ilianza kupanda, sababu makampuni na mataifa yalianza kupunguza roder za kununua mafuta kutoka Iran, na Iran wakaanza kupunguza uzalishaji.

2. Baada ya Saudia kutangaza kuongeza uzalishaji, bei ya mafuta imeshuka, maanake manunuzi yanaelekeswa Saudia.

3. India imeishashusha uagizaji wake wa mafuta kutoka mapipa 500,000 kwa siku mpaka mapipa 300,000.

4. Makampuni makubwa ya usafishaji mafuta ya nchini China, hayajaweka order ya kununua japo tone la mafuta ya iran kwa mwezi wa kumi na moja, hali hii inategemewa kwa miezi ifuatayo.

5. Bank mmoja nchi china ambayo ilikuwa inaprocess transactions za wafanyabishara wa mafuta wa iran, imewaeleza wateja wake hao kwamba ikifika tarehe nne nov, hakutakuwa na huduma kwao.
 
Back
Top Bottom