Mara nyingi taarifa ya ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari ama ikibidi pamoja na ndugu. Taarifa iliyotolewa ipokelewe ilivyo. Hata wakitujuza kwa namna nyingine hatutaamini tunachoambiwa hasa tukiwa tayari na fikra ya kuamini kuwa kisemwacho sicho, na tunachokihisi ndicho. Tuwe na sibira.