GE2025 Vigogo CCM wapita 'chocho' kwa 'chocho' kusaka kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
MGOMBEA nafasi ya udiwani wa Kata ya Mbweni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulkadir Mgheni, ameendelea na kampeni zake leo akishirikiana na vigogo wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Mkoa, Shyrose Bhanji.

Viongozi hao kwa pamoja wameungana na Viongozi, wanachama wengine wa ngazi za Wilaya, Tawi na Shina kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba, maarufu kama 'chocho kwa chocho,' ili kuhakikisha kura za CCM zinapatikana kwa nafasi zote - udiwani, ubunge na urais - kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Your browser is not able to display this video.
 
Na bado hata kama wakiomba ardhi ipasuke ili wapite chini kwa chini.Hata hivyo baada ya kupita njia hizo watakuja hapa na kutudanganya lami hadi vichochoroni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…