Nakumbuka ilikuwa siku flani ya mwanzo wa kikupwe, mwezi wa sita miaka hiyo ya 90's.
Ilikuwa ni asubuhi ya saa kumi na mbili, ni siku nisiyoisahau.
Ingawa tulikuwa na taarifa ya nini kitatokea siku nne zijazo, ile asubuhi zile mishemishe zake zilituogofya sana. Tuliamshwa na mzee, na
tukapewa GR na mwelekeo. Tukafika, tukawakuta wenzetu pia.
Tukakutana na ngariba wa Kimatumbi, tukapigwa timbwili la nguvu, bila ganzi, bila kushikiliwa, goma likaisha. Wa kulia walilia, wa kukomaa tukakomaa, goma likaisha. Baada ya siku zisizozidi saba, kidonda kikapona, maisha yakaendelea.
Kuenzi hii kitu, wiki iliyopita mtoto wangu wa kwanza naye nimempa doso la asubuhi kweupeeee, kavukavu bila ganzi, ila leo kashapona na yupo sawa kabisa. Kitu cha bila ganzi kidumu.....kidumu!