Andika heading ya thread yako vizuri. Kuandika tuu "video" ndio nini kama si kutaka watu wairuke thread thread kwa kudhani ni zile zile ambazo hazina mpango? Pia kwenye maelezo yako fafanua unatumia PC ya aina gani, unatumia Operating system ipi, kama unashindwa kuangalia video za kwenye internet au zilizomo kwenye hiyo PC, unaangalia video za kwenye internet speed ya connection yako ikoje na unatumia browser ipi, kama unaangalia video zilizomp kwenye PC unatumia video player ipi, n.k