Vichaa kutoka asylum moja wanapelekwa nchi jirani kwa ndege kucheza mechi ya kirafiki na vichaa wenzao huko.
Kwenye ndege hakukaliki,mara huyu kamrushia mwenzie mpira,mara huyu ka inflate life jacket basi tabu tu.
Kocha kajaribu kuwatuliza ikashindikana,lakini kuna kichaa mmoja yeye alikuwa ametulia anasoma gazeti.Kocha kachoka kaamua kwenda seat ya mbele akalala.
Mara kocha kustuka anaona ukimya umetawala kwenye cabin,akaamua ageuke nyuma.Huko nyuma kamwona yule kichaa aliyekuwa anasoma gazeti.Ikawa kama hivi
KOCHA:We! wenzio wakwapi?
KICHAA:Nimeona wanakusumbua nimefungua mlango nikawatupia mpira wakachezee nje.