Inabidi uandike parser, yaani program itakayoisoma file ya vb kisha kuigeuza kuwa php kwa kutumia rules fulani, unaweza kuiandika hiyo parser kwa kutumia vb yenyewe. So utasoma text file ya code ya vb, e.g. ukikutana na line yenye structure ya "<access level> Function <name> (<parameters>)" unajua huu ni mwanzo wa function na unachukua kuanzia hapo mwanzo hadi mwisho wa function "End Function".
Kwa hiyo kazi yako ni ku indentify code ya vb inasema nini kisha kuigeuza kuwa php. Hili unaweza kufanya simply kwa kutumia if statements au jaribu kuangalia regular expressions kufanya pattern matching.
Same kwa ajili ya GUI ila hapa panakuwa pagumu, maana format ya layout file za Vb.net (Win forms) ni complicated sana.
Kuna vitu ambavyo havina translation kama program yako ilikuwa imetengenezwa kwa ajili ya windows specifically, ila functions ambazo ni business logic sidhani kama kuna ambayo inashindikana technically kuandikwa kwa PHP.