Valentine day imekaribia

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Haya haya kumekucha,ile siku ya wapendanao imekaribia.Kwa wenye mapenzi ya msimu na matukio maalum muda wenu wa kuumiza vichwa kwa ajili ya zawadi na namna ya kutoka.

Kwa wale wenye mapenzi ya dhati yasiyo ya msimu ni siku ta kawaida kama siku zingine.Kwa wale wenye kutoka na michepuko badala ya wake zao na kuongopa wanaenda safari za kikazi nje ya mji haya.

Maandalizi mema.
 
kishkwambi shoga angu we utatoka wap sasa??? Sjui ntoke na babe wangu Bulldog au sio babe??
 
Last edited by a moderator:
Duuh ama kweli WATZ na waafrika kwa ujumla wetu tuko vilaza. Hata kubuni sikukuu /siku Maalum za kijamii mpaka "tukopi & kupesti".
 
Duuh ama kweli WATZ na waafrika kwa ujumla wetu tuko vilaza. Hata kubuni sikukuu /siku Maalum za kijamii mpaka "tukopi & kupesti".

Hata hivyo tulivyocopy and paste hatuvielewi tunajifanyia madudu tu. Mi hata nashangaa waafrika wako na valentine ati sijui haloween day looh!
 
kila la kheri kwa wote wanaoitukuza siku hiyo kwa anasa......
 
Sikukuu hii imekosa mvuto tangu penzi lilipoanza kununuliwa......
Wakati kiuhalisia penzi la kweli hutoka moyoni na sio mfukoni....
 
Sikukuu hii imekosa mvuto tangu penzi lilipoanza kununuliwa......
Wakati kiuhalisia penzi la kweli hutoka moyoni na sio mfukoni....

hapa umeongelea kwa wanawake tu ....na je kwa wanaume wanaothamini mwonekano wa nje je.......?
 
hapa umeongelea kwa wanawake tu ....na je kwa wanaume wanaothamini mwonekano wa nje je.......?

Kwani hakuna wanawake wanawarubuni wanaume kwa fedha na kuwaacha wapenzi wao waliowapenda na kufuata fedha...??
THINK BIG
 
Kwani hakuna wanawake wanawarubuni wanaume kwa fedha na kuwaacha wapenzi wao waliowapenda na kufuata fedha...??
THINK BIG

sijakataa ulichosema.....ila umegusa upande mmoja......mapenzi hayajaalibiwa na wanawake tu kwa kupenda pesa......
 
sijakataa ulichosema.....ila umegusa upande mmoja......mapenzi hayajaalibiwa na wanawake tu kwa kupenda pesa......

Ukiutumia ubongo wako kufikiria utaelewa ninacho maanisha....ninamaanisha wale wote wanaotumia fedha kumpata mpenzi haijalishi awe mwanamke au mwanaume..yeyote kati yao aliyetumia fedha kujipatia penzi ni kwamba anakuwa ameharibu maana nzima ya penzi...kwani penzi la kweli hutoka moyoni na sio mfukoni...kwa maana ya penzi la kweli watu hawashangai kuona mtoto wa kishua anahama kwao kwenye kila kitu..na ana hamia kwa msela asiye na mbele wala nyuma....kwa maana ya penzi la kweli haishangazi kusikia mtu anauza vitu vyake na kuhamia kwa ampendae....
Kumbuka kwenye bandiko langu la kwanza sijataja jinsia....
Natumaini umenielewa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…