Sijui unaongea nini ndugu yangu ?
thread hii inahusu zinaa, Nawashauri ndugu zangu pamoja na kuishauri nafsi yangu kuaacha zinaa.
Zinaa maana yake ni kufanyana baina ya watu wawili ambao hawakuoana kisheria. Madhara ya uzinifu ni makubwa ikiwa ni pamoja na kuleta fitina, ugomvi na hata kuuwana. Maradhi yanayoletwa na uzinifu ni makubwa na ambayo hayaponeki. Madhara katika jamii ni makubwa na mabaya ambayo inafikia kiwango cha kaka kumuoa dada kwa kutokujua baba zao au asili yao.
Anaemzini mke wa mtu anakuwa kamfanyia dhulma mumewe, na ikiwa kashika mimba basi mtoto anaezaliwa huwa si miongoni mwao. Na ikiwa kamzini msichana hajaolewa akizaa mtoto wa haramu huwa kamwangamiza maisha yake na mustakbali wake. Na pia kamvunjia heshima yake na ya wazazi wake. Na zina imefananishwa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu S.W.T. kwa sababu SHIRKI ni dhulma kubwa.