UZALENDO KWANZA!!!!!!

muda wa ukombozi

Senior Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
129
Reaction score
118
Inaandikwa na MUDA WA UKOMBOZI

Kuna mambo ambayo ni kweli yanatia sana uchungu, hasa nikikumbuka ule ugomvi wa kitoto ambao wakati wa ugomvi, ndondi zimekolea na wakati mwingine unaelekea kushinda alafu unakuta watu wanaojifanya wasamaria wanakuja kuamuria ugomvi ule kwa kukushika madhubuti peke yako huku mwenzako akiwa huru nakuendelea kukupiga anavyotaka.

Yaani nilikuwa naumia sana hasa kupigwa na mtu ambaye naamini hana uwezo wa kusimama na mimi Yaani mtu beee!!! inauma sana kwa maumivu hayo unajikuta pia upo mahabusu au kwenye adhabu zingine kwasababu tu ya kupigana na mtu ambaye anaangaliwa kama taa au yai na watu wake.

Yaani mi ningelipenda uwanja huru wa hoja, pale ambapo kuna kitu chema kwa manufaa ya nchi limefanywa au kinatarajiwa kufanywa hatuna budi kuwa kitu kimoja kutekeleza hilo, kinyume chake pia turuhusiwe kwa hadhi ile ile ya kuwa kitu kimoja katika kutokukubaliana kwenye misingi ya hoja kwa maendeleo ya Taifa.

Tuache ushabiki kwenye masuala nyeti ya nchi yetu, pale ambapo serikali inabidi ikosolewe iwe hivyo kwa maendeleo ya nchi kama ilivyo kwenye serikali ikisifiwa tupige makofi kwa kuipongeza.

ila ushauri wangu tukikubali kuwa tunasifia tu, tutakuwa hatuna tofauti na jamii yenye utindio wa ubongo au kuna komredi flani anapenda kuwaita mazwazwa au nyumbu kwa maana tutakuwa jamii ya waoga, jamii isiyopenda kushiriki maendeleo ya nchi yao bali inayopenda kuletewa chochote kiwe kibaya au kizuri na viongozi wao waliowapa dhamana, jamii ambayo wanahisi viongozi waliowachagua ni miungu watu, viongozi hawakosei na akitokea mkosoaji jamii hiyo wanampinga huyo.......!!!! ikiwezekana kumtenga kwasababu kupinga sio desturi yao....!! Kama utakuwa umepata bahati mbaya kuwa kwenye jamii hiyo! Sahau kuhusu maendeleo kabisa.

Tukiwa tunasema keki ya Taifa tunamaanisha ya kila mtanzania anapaswa aifurahie kwa namna yake, watawala wakati wanaila inabidi waweke mazingira mazuri na watawaliwa waionje japo kidogo kupitia uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kutoa maoni na kuishauri serikali kwa jinsi utakavyoona, uhuru wa kufanya siasa kwa vyama vilivyosajiliwa na kutambulika bila kunyanyaswa lakini kikubwa huu sio ule wakati ambao tuliambiwa watanzania hawaitaji uhuru bali wanachokitaka ni chakula, madawa hospitali na vitu msingi tu "neccessities", hapana hatupo kwenye huo wakati, watz tunahitaji watawala wafuate msingi wa utawala bora bila kusahau haki za binadamu "fundamental of human rights" tusiruhusu wa Tanzania wawe waoga ndani ya nchi yao, tutatengeneza kizazi ambacho wakati sisi tupo wazee tutachukia na kuwalaumu kwa kile ambacho kitakuwa kinaendelea.

Tumuunge mkono yule tu anayeonekana ni mzalendo anayepambana na uhuru wa habari, anayekemea ufisadi, asiyetaka kukandamizwa kwa uhuru wa haki za binadamu, kubakwa kwa uhuru wa vyama vya siasa.

Tumuunge mkono yule anayepambana ili Tanzania iwe mpya na kuziba mianya ya kuitwa shamba la bibi.

muda wa ukombozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…