Uwazi wa mikataba

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,348
Reaction score
1,466
Mwenye mkataba kati ya Dangote Cement na TPDC kuhusu makaa ya mawe naomba anisaidie niupate.

Pia mkataba kati ya Dangote Cement na TPDC kuhusu gesi wa miaka 20 pia nauomba.
Tuanze kuangalia mapema isije ikawa tumeliwa baada ya miaka 12 tuanze kutafuta sifa.
Sijajua kwanini Dangote Cement wanaweka masharti sana kwenye kufungua kiwanda chao kwasababu tumekua na viwanda zaidi ya viwili vya Cement na hawajawahi kusita kwasababu ya gesi au makaa ya mawe. Kwasababu kama kuna tatizo la nishati, tungeanza kuvisaidia viwanda ambavyo vipo katika uzalishaji tayari, twiga wanauza mfuko sh 10000- 15000 pamoja na matatizo haya ilitakiwa ndo wawe kipaumbele, (labda matengenezo yao mapya ndo yanahusu kuingiza gesi) ila yote kwa yote hawa ndo walitakiwa kutuendesha sio mgeni.

Tusaidiane jamani, gesi yetu ni mpya ikianza kupigwa mapema hivi watu wetu hawataacha kutumia mkaa wala kuni.

Mwenye mkataba alete hapa tutoe kasoro.
Naiamini serikali na nia yake njema, lakini imani hii imefanya tuliwe sana kwenye madini.
Miaka 20 ni mingi sana aisee, ni mihula minne ya uongozi wa uchaguzi mkuu, bora kila mtu ajue toka mwanzo kabla mambo hayajaharibika.

Inawezekana viongozi wetu hawajui ku-negotiate ndomana katika kila mkataba tunaliwa, sasa ili kuepuka kuliwa mambo yawe hadharani ili mwenye kujua a na mwenye kujua ze wote waone na wachangie.

Nchi ya watu milion 50 kulilia mkono wa Dangote ni fedheha.
Kuna haja gani ya kujisifia kwamba katika miaka 5 tuliwezesha kiwanda cha Dangote kufunguliwa wakati gharama yake ni kuliwa kwa miaka 20? Badala ya kufanya hivyo serikali ingeongeza mitaji kwenye viwanda vya Cement vilivyopo vikaongeza ufanisi na ajira zikaongezeka na vikauza Cement hata kwenye nchi za jirani kama burundi na ukifanya shilingi yetu kuwa na nguvu.

Miaka ishirini mingi sana aisee, tukiliwa na kwenye huu mkataba kwa miaka ishirini hatutakua na namna bora tukubali uchumi wetu utawaliwe na mashrika kwasababu kama nchi tutakua tumeshindwa.

Mimi kama wananchi wengine wanaomuamini Ndugu Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tupo tayari kuipigania kila shilingi ya hii nchi, serikali ifanye mambo kwa uwazi ili hata ikishindwa wote tuwe tunaelewa.
 
Inawezekana tukaipa Dangote Cement gesi kwa gharama nafuu lakini simenti yenyewe ikawa inauzwa nje ya nchi tena kwa faida ambayo haitainufaisha mamlaka ya mapato.
Sisi tukabaki kusifia ajira wakati twiga wangeongezewa mtaji wangezalisha zaidi nchini na kukuza ajira simultaneously.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…