Shida kubwa ni ubinafsi kwa viongozi wivu wa viongozi wengi kufikiri hakuna anayestahili kulipwa zaidi yao ni hilo tu.wazungu wawekezaji wengi wamekuwa wakiwashangaa sana hawa viongozi.wawekezaji waliona basi ni afadhali walipe kwa dola angalau mtanzania apate angalau kidogo, wakaamua kuondoa na kudai kulipwa kwa dola kunaleta mfumuko wa bei.
Jamani,hawa watanzania wenzetu wakilipwa vizuri si ndiyo mwanzo na wafanyakazi wa serikalini kulipwa vizuri kwa ongezeko la kodi hii ya wafanyakazi wa migodini.
Ukweli ni kwamba tanzania ni nchi ambayo ingeweza katika kampuni nyingi watu kulipwa si chini ya kima cha chini cha milioni mbili kwa mwezi,tatizo ni uchoyo,wivu na ubinafsi,madhalani makampuni ya simu ambayo yanaingiza faida ya mabilioni ya pesa,makampuni ya pombe,makampuni ya sigara,makampuni ya madini na uchorongaji/drilling companies,bima ,makampuni ya ujenzi wa barabara,mabenki nk.shida nyingine ni kujipendekeza viongozi wetu kwa wawekezaji pamoja na ufisadi ambapo kuna makampuni kama vile voda nk ambayo wakubwa weingi ni wazamini.
Nini cha kufanya ni juu yetu kutafuta mustakabali wetu.