muache aende wala asiogope!!! me ilinitokea issue kama hiyo mwaka 2010, secretariate ya ajira waliniita lakini sikuwa na cheti bali transcript. ilinihudhunisha sana na ilinibidi niombe ushauri kwa watu mbalimbali wengine walinambia bora nisiende maana sitaruhusiwa kuhudhuria interview au wanaweza kuniruhusu interview lakini ajira nisahau!! Ila kuna mwalimu wangu wa chuo alinipa moyo sana aliponambia wewe nenda wakakurudishe wenyewe badala ya kujirudisha wewe binafsi, zaidi ya yote akasema transcript kwa Muajili muelewa ni Nzuri maana inaonyesha actual score katika kila soma alilofanya Muhusika. Kweli nilienda na transcript zangu hawakunirudisha nikafanyiwa interview baadae nikawa miongoni wa walioitwa kazini na mpaka sasa nipo kazini.
Cha muhimu ukipata kazi fanya juhudi uchukue cheti chako mapema ili utakapoitwa kuripot kazini uwe nacho!
nakutakia Interview njema..!!!!!!!