wewe usijisumbue kwenda PCCB wale wananuka na siwapendi kabisa, tulifanya interview pale PCCB kwenyewe wameitwa watu kwenye ajira wanane ambao kwa hakika hawakuwa shortlisted na siwajui kabisa,na tulipeleka malalamiko tukachinjiwa baharini hakuna aliyethubutu kuwafuatilia kwani mwisho wa siku tukaambiwa ni watoto na wajomba za watendaji wa serikali na wafanyakazi wa PCCB, aidha kuna mmoja alikuwa anatamba kwa kumwambia rafiki yake tunayefahamiana kuwa alikuwa anasoma CPA hajaamua aende depo au lah lakini mwisho wa siku amekwenda na yuko kazini sasa, kwa ufupi serikalini pameoza kabisa na tunahitaji mabadiliko kibao,nilikuwa kwenye interview hiyohiyo na masters yangu eti mtu ananiuliza nitaje majina ya mawaziri 10 waliowahi kushika wizara ya mali asili na utalii, then nitaje sababu zilizofanya waondoke wote,afu mtu anakuzomea palepale.