habar zenu wakubwa kwa wadogo
Napenda tukumbushane mambo ambayo wazazi wetu walikua wakitudanganya pindi bado tupo wadogo.
Mimi naanza kama ifuatavyo
(a) mzazi wangu alifanikiwa kunidanganya kuwa kwenye page za biblia sehemu ambayo iko plain basi ujue kuna dhambi nimetenda so ndo maana maandishi yamefutika.
Hapa niliogopa sana
(b)siku tukila mahindi iwe ya kuchemsha ama ya kuchoma,bas ataomba anioneshe njia (kula mhindi) basi na mm bila hiana hutoa bila kinyongo
(c)kuangalia movie za ki Nigeria zile za kichawi niliogopa sana ,kwa sababu mzazi aliniambia nikiangalia wataniijia usiku.
Wazazi zamani walitumia njia kama hiyo (a) ili kumfanya mtoto aheshimu maandiko katika biblia pia na kumheshimu MUNGU aliyejuu
Hebu na ww mwana jf mwenzangu tuambiane wazazi wako walitumia njia gani & walikudanganya namna gani?