Utofauti wa majina

Joseph5

New Member
Joined
Jan 19, 2023
Posts
3
Reaction score
8
Naomba ambaye alishawahi kukutana na hii changamoto afafanue aliisolve vipi majina katika vyeti yanatofautiana na majina ya kitambulisho Cha taifa
 
Namaanisha vyeti vya shule vinasomeka kwa majina mawili tu lakini NIDA Kuna majina matatu mfano Kwenye vyeti Hamis Isdor,lakini Kwenye NIDA ni Hamis Isdor Abel
 
Naomba ambaye alishawahi kukutana na hii changamoto afafanue aliisolve vipi majina katika vyeti yanatofautiana na majina ya kitambulisho Cha taifa

Hujaelezea changamoto yako kwa uwazi kwa hiyo ni vigumu kutoa ushauri.

Mfano
-ungetuambia huo utofauti wa majina ukoje?
-unapata au umepata shida gani kutokana na huo utofauti?
-ni vyeti gani vimetofautiana majina na NIDA yako?

Elezea shida yako vizuri ili usaidike/upewe ushauri badala ya kuhojiwa maswali

Kila la kheri.
 
Namaanisha vyeti vya shule vinasomeka kwa majina mawili tu lakini NIDA Kuna majina matatu mfano Kwenye vyeti Hamis Isdor,lakini Kwenye NIDA ni Hamis Isdor Abel
Hao ni watu wawili tofauti.Kama unataka awe ni mtu mmoja,nenda RITA wakakuelekeze cha kufanya.
 
Kila siku mnaanzisha uzi wa aina hii, em jaribuni ku-search mana humu kuna nyuzi kibao khs hayo
 
Mbona hakuna utofaut hapo si jina tu limeongezeka mwanzo halikuepo mimi nimesomea majina mawali tu lkn ninapolazimika kuongeza la ukoo naongeza sijawah kua na changamoto
 
Nenda kwa mwanasheria akuandalie document ya kubadilisha jina unakwenda wizara ya ardhi unaisajili shughuli kwisha
 
Nenda kwa mwanasheria akuandalie document ya kubadilisha jina unakwenda wizara ya ardhi unaisajili shughuli kwisha
Wizara ya Ardhi tena ? au mie ndio nina wenge la usingizi maana ndo naamka hapa.....
 
Andaa bajeti anbayo haipungui 100K
Kisha nenda kwa Mwanasheria

Ardhi
Gazeti
N.k
 
Hapo inabidi uonane na mwanasheria akupe muongozo maana itabidi uende Court kuapa na kukiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…